Sasa katika kuchungulia kwangu huko Instagram ili nione nini cha kuwaleta hapa, sinikakutana na page ya Madam Rita Paulsen. Nikaamua kuipiga chabo kidogo ?? Mbali na picha zake nzuri nikaona videos clips mbalimbali, nyingine Charles Hillary akicheza. Basi nikaamua kuitazama kwakuwa ilikuwa fupi nikasema ngoja niende kwa YouTube nikaiangalie zaidi. Dah! Si ndio nakutana na hii interview yake alifanya na Mkasi. Hivi kwanza, Mkasi bado ipo au imekufa? Mimi sijui, hata ile Bongo Star Search sijui kama bado ipo. Au ni mimi ndio niko nyuma ya ratiba ?? btw, mimi ni TV addict! Yani kitu Radio hata sijawahi sikiliza unless nipo kwenye gari la mtu au nyumba ya mtu that I'm NOT free enough kusema zima ?? tofauti na mdogo wangu Magreth na dada yangu Elline hawa wawili na Radio huwatenganishi Anyway, back to our story.......Sasa katika kujieleza nikagundua kuwa kumbe naye kama mimi! Alizaa akiwa underage (only 14 yrs old). Dah! Amenigusa sanaaaaaa! Can you imagine having a baby at 14 yrs old?! Jamani, hivi vitu visikie tu kwa mwingine yasikukute! Kama mimi kuzaa at 18 yrs old, nilichekwa na kudhihakiwa hivi yeye aliyezaa at 14 ilikuwaje!! I feel like I wanna hear more about it! Embu msikilize mwenyewe ?
Sasa huyu Madam Rita, mbona sikusikia akipaza sauti yake kuhusu kauli ya kuzuia watoto waliopata mimba kwenda shule? Akaniacha mimi kidogo nimtoe "roho" mama yangu kipenzi mama Salma Kikwete ?? Madam Rita kama utasoma hapa please we need you to be the voice of the voiceless. Denzel Washington anasema, "don't just aspire to make a living, aspire to make a difference". Tafadhali amka madam. Nimependa your new talk show. So nice!