Binafsi nilikuwa sijawahi msikia John Akwari mpaka juzi kati nilipokutana na hiyo ?post hapo juu. Labda nianze kwa kusema kuwa kwenye maswala ya michezo ukitoa netball, basketball, tennis, na swimming kwakweli mie si mpenzi sana wa michezo. Hivyo huwa siifatilii sana! Kwasababu hiyo ni utetezi tosha wa kwanini simfahamu John Akwari. Au pia niseme taifa letu limeshindwa kuwaenzi watu kama John Akwari na ndio sababu watu wengi hatumfahamu!…………..Lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kumuweka hapa. Sababu kuu nikutaka watu waguswe na habari ya huyu shujaa wetu ambaye sisi tumeshindwa jivunia wakati mataifa mengine wanajivunia na kuguswa kwa ushujaa wake!………… Najua maisha yana changamoto nyingi ambazo wengi wetu tunapitia. Na saa nyingine mateso na maumivu yanakuwa makali sana kiasi cha kutaka kukata tamaa ya kutimiza ndoto zako au kuendelea na maisha. Trust me, I’ve been there multiple times! I truly understand and know the feeling! Basi usife moyo, kuwa mshindi si kuwa wakwanza kufika bali the spirit of not giving up is the real victory! …….. Embu tazama hii video
Nilijaribu kutafuta habari yake na nikakutana na haya ?mahojiano ambayo amefanya na Issa Michuzi soma hapa ? Michuzi …….. Acha kifo ndio kiamue kuwa ndoto zako zimefika ukingoni lakini wewe kazana tu! Kama unahitaji kupumzika basi fanya hivyo! Vuta pumzi ukipata nafuu endelea na safari. Wengi tunaonekana tunatembea kiushujaa kabisa japo miyoyo yetu ina ‘chechemea’ kama matone ya drip kutoka na mambo ambayo tumepitia au tunapitia.
One thought on “Je, wamfahamu John Stephen Akwari?!”