Kagua mazingira kabla ya kuondoka!

FB_IMG_1458313806744Wapendwa, naomba nikumbushe swala la kukagua mazingira ya tulipo kabla ya kuondoka. Kwa mfano angalia hiyo picha juu jinsi mtoto alivyo jificha. Sasa mtu kama hatojali kukagua mazingira yake kabla ya kuondoa gari inamaana mtoto huyu anaweza poteza maisha yake.

Haya mambo yameshatokea sana. Na ndio maana nakumbushia. Hata kama wewe hauna mtoto hakikisha kuwa unaangalia kabla ya kuondoka kwani huwenda mtoto wa jirani yako yupo kwenye hatari. Tena hakikisha unasema / uliza kwa sauti ili hata kama mtoto hajakuona basi atasikia sauti ikiuliza kama kuna mtu.

Kagua hata majiko (umeme / gas) ndani ya nyumba yako kabla ya kuondoka uwezi jua haswa kama unawatoto ndani. Usiweke vitu ovyo ovyo kwani ni hatari sana. Kwa mfano dawa au hela za chumba ambazo mtoto anaweza meza. Kuwa sensitive na mazingira kwa usalama wa watoto na pia wako mwenyewe.

Leave a Reply