Watanzania wengi siku hizi wamekuwa na tabia ya kutaka kulazimisha kila mtu mwenye uwezo au mfanyabiashara mkubwa awe "mwanasiasa" au "mwana harakati wa siasa" kitu ambacho siyo sahii hata kidogo! Siyo kila raia wa Tanzania anatakiwa kujihusisha na siasa! Hapana! Kuwa kwenye siasa au ku support chama fulani hayo ni maamuzi binafsi, na biashara ni mtu binafsi! Mmiliki wa biashara ana hiyari ya kujihusisha moja kwa moja na siasa au akakataa, na lazima kila mtu haeshimu maamuzi yake! Unapoanzisha biashara unless ni biashara ya "siasa" then utalega kupata wanasiasa otherwise unafungua biashara kwaajili ya kuhudumia watu wote bila kujali itikadi zao! Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji! Nasema hivi kwasababu watu wengi ambao mnalaumu baadhi ya wafanyabiashara ukiwachunguza utagundua kuwa hawajahi kujaribu kutengeneza kitu chochote au kuangaika from the scratch mpaka kitu kikatembea na watu wakaona ndio maana hamuwezi jua thamani ya kupoteza kitu chako ulicho kiangaikia wewe mwenyewe toka chini! Hamuwezi jua mtu alijinyima kiasi gani ili apate kitu chake mwenyewe! Hamjui mtu huyo alifunga na kuomba Dua kwa muda gani ili Mungu ambariki na biashara yake! Hamjui ni mara ngapi amelia akiona ndoto yake haifanikiwi! Halafu leo hii akubali tu kirahisi rahisi kuharibu mali zake kwasababu ya siasa?! Kuna njia nyingi za kushiriki kuleta amani na maendeleo katika nchi yako bila kujiingiza kwenye siasa!
Siyo kila mtu anajali nani yupo madarakani, wengine wanachotaka ni amani kwani wanajua gharama ya kukosa amani! Msilazimishe kila mtu awe mwanasiasa au mshiriki wa chama fulani kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi yake na jinsi ya kuendesha maisha yake! Sasa leo mkilazimisha kila mtu awe mwanasiasa then what next? Mtakuja kulazimisha kila mtu awe Muislamu au Mkristo? Nahata katika ukristo bado kuna madhehebu, sasa itakuwaje? Mtakuja kulazimisha wakristo wote wasali Roman? Unafikiri mimi ambaye ni Msabato nitakubali?! Wakati najua thamani na raha ya kuwa Msabato!! ........ Embu acheni ujuaji usiyo na kichwa wala miguu! Mpaka siku ile utajifunza jinsi ya kubeba maji yako mwenyewe kutoka mtoni hauto kaa ujua gharama ya kumwagika kwa tone la maji!
Related