*KESHA LA ASUBUHI*
JUMATANO
09/05/2018
*_ANAJIBU MAOMBI YA KUTAKA MSAADA WA MUNGU _* ? _Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Kumbukumbu 6:6, 7_.
✍?Akina baba na akina mama, nitawezaje kupata maneno ya kuelezea jukumu lenu kubwa! Kwa tabia mnayoidhihirisha mbele ya watoto mnawafundisha kumtumikia Mungu au kuitumikia nafsi. Basi toa maombi yako ya dhati kwa mbingu kwa ajili ya msaada wa Roho Mtakatifu, ili mioyo yenu ipate kutakaswa, na kwamba njia mnayoifuata iweze kumheshimu Mungu na kuwavuta watoto wenu kwa Kristo.
✍? Inapasa kuwapa wazazi hisia ya umakini na utakatifu wa kazi yao, pale wanapotambua kuwa kwa mazungumzo au matendo ya kizembe wanaweza kuwapoteza watoto wao.
✍?Wazazi wanahitaji uongozi wa Mungu na Neno lake. Wasipoyasikiliza mashauri ya Neno la Mungu, wasipofanya Biblia kuwa mshauri wao, kanuni ya maisha, watoto wao watakua wakiwa wazembe na watatembea katika njia za kutokutii na kutokuamini.
✍? Kristo aliishi maisha ya kazi na kujikana nafsi, na alikufa kifo cha aibu, ili apate kutoa mfano wa roho ambayo itawachochea na kuwatawala wafuasi wake. Kadiri ambavyo wenzi wa maisha wanajitahidi nyumbani kwao kufanana na Kristo, mvuto wa mbinguni utaenezwa katika maisha ya familia yao.
??♂```Katika kila nyumba ya Kikristo Mungu anapaswa kuheshimiwa kwa dhabihu za asubuhi na jioni za sifa na maombi. Kila asubuhi na jioni maombi ya dhati inabidi yapande kwa Mungu kwa ajili ya baraka na uongozi wake.
Je Bwana wa mbingu atapita katika nyumba kama hizo na asiache baraka hata moja pale? Hapana, kwa kweli.
??♂ Malaika wanasikia utoaji wa sifa na maombi ya imani, na wanabeba maombi kwenda kwake yeye anayehudumu katika patakatifu kwa ajili ya watu wake, na kukiri ustahili wake kwa niaba yao. Maombi ya kweli hushikilia nguvu za Mungu na kuwapa watu ushindi. Juu ya magoti yake Mkristo anapata nguvu ya kupinga jaribu. - Review and Herald, Feb. 1, 1912.```
*MUNGU TUWEZESHE KUTAMBUA KIMBILIO LETU NI WEWE TU*
Related