KESHA LA ASUBUHI
IJUMAA
18 MAY 2018
*Anakwenda Nyumba kwa Nyumba Pamoja na Watendakazi wa Injili* ? _Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa. Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. Na nyumba yo yote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini. Luka 9:1-4._
✍?Bwana anawaita watu wake kuchukua njia mbalimbali za huduma za umisionari. Wale walioko katika njia kuu na walio katika sehemu zisizofahamika vizuri katika maisha wanapaswa kusikia ujumbe wa injili. Washiriki wa kanisa wanapaswa kufanya kazi ya uinjilisti katika kaya za majirani zao ambao bado hawajapata ushahidi mkamilifu wa ukweli ulio kwa ajili ya wakati huu.
✍?Hebu wale ambao wanachukua kazi hii wafanye maisha ya Kristo kuwa somo lao la kudumu. Hebu na kwa bidii sana, wawe wanatumia kila uwezo katika huduma ya Bwana. Matokeo yenye thamani sana yatafuatia juhudi za dhati zisizo na ubinafsi. Kutoka kwa Mwalimu mkuu watendakazi watapokea elimu ya juu kabisa kuliko zote. Lakini wale ambao hawagawi nuru hii waliyoipokea siku moja watatambua kuwa wamepata hasara ya kutisha.
✍? Wengi wa watu wa Mungu inabidi watoke na machapisho kwenda katika sehemu ambazo ujumbe wa malaika wa tatu haujatangazwa. Kazi ya mwinjilisti wa vitabu ambaye moyo wake umejazwa na Roho Mtakatifu imejaa uwezekano wa ajabu wa mema. Uwasilishaji wa ukweli, katika upendo na usahili, kutoka nyumba moja hadi nyingine, unapatana na maelekezo aliyotoa Kristo kwa wanafunzi wake alipowatuma katika safari yao ya kwanza ya umisionari. Kwa nyimbo za sifa, maombi ya dhati, na uwasilishaji sahili wa ukweli katika familia moja, watu wengi watafikiwa.
✍? Mtendakazi mtakatifu atakuwapo kupeleka usadikisho kwa mioyo. “Mimi niko pamoja nanyi siku zote” (Mathayo 28:20) ndio ahadi. Kukiwapo uthibitisho wa uwapo wa kudumu wa Msaidizi wa jinsi hiyo, tunaweza kutenda kazi kwa imani na tumaini na ujasiri.
??♂```Ukinaifu wa huduma yetu kwa Mungu unapaswa kuvunjwa. Kila mshiriki wa kanisa anapaswa kujiingiza katika huduma fulani maalum kwa ajili ya Bwana.
??♂ Hebu wale ambao wamejiimarisha katika ukweli waende katika sehemu jirani, na kufanya mikutano. Hebu Neno la Mungu na lisomwe, na hebu mawazo yanayoelezwa yawe katika jinsi ambayo yataeleweka na wote bila shida. - Review and Herald, May 5, 1904```.
*MUNGU AKUBARIKI*
Related