Kesha la asubuhi: Anaongoza Utakaso wa Familia

                   *KESHA LA ASUBUHI*

                 _ALHAMISI MEI 10, 2018_

           *Anaongoza Utakaso wa Familia* _Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Mithali 22:6._

? Ninawasihi wazazi kujiweka tayari wao wenyewe na watoto wao kujiunga na familia ya juu. Kaa tayari, kwa ajili ya Kristo, kaa tayari kukutana na Bwana wako kwa amani. Anza kufanya kazi katika familia yako kwa namna itakayoleta matokeo mema. Anza katika mzizi wa jambo lenyewe. Leteni ukweli katika nyumba zenu, ili kuwafanya kuwa watakatifu na kuwatakasa. Usiuache katika ua wa nje. Ni vipofu kiasi gani wale wanaodai kuwa Wakristo kuhusu maslahi yao wenyewe! Ni kiasi gani wanashindwa kabisa kuona kile ambacho Kristo angeliwatendea iwapo angeliruhusiwa kuingia katika nyumba zao.

? Hebu Wakristo na watende kwa bidii ili kupata taji ya uzima kama vile walimwengu wanavyotenda ili kupata manufaa ya kidunia, na kanisa la Mungu kwa hakika litasonga mbele likiwa na nguvu. Roho Mtakatifu hutoa matendo ambayo yanapatana na sheria ya Mungu. Kazi ya kuhuisha ya Roho itaonekana katika familia zenye kujitahidi ili kuonesha wema, uvumilivu, na upendo. Uwezo wenye nguvu zote uko kazini, ukiandaa akili na mioyo ipate kujisalimisha kwa uwezo unaoumba wa Roho Mtakatifu, ukiwaongoza wazazi kujitakasa wao wenyewe, ili watoto wao pia wapate kutakaswa.

? Nyumba ambayo washiriki wake ni Wakristo wapole, waungwana huweka mvuto wenye ushawishi mwingi kwa ajili ya wema. Familia zingine watazingatia matokeo yaliyopatikana na nyumba kama hizo, na watafuata mfano uliowekwa, kwa upande wao wakilinda kaya zao dhidi ya mivuto ya kishetani.

? Malaika wa Mungu mara nyingi watatembelea makazi ambayo ndani yake mapenzi ya Mungu yanatawala. Chini ya nguvu ya neema ya Mungu kaya kama hiyo inakuwa ni mahali pa kuburudisha kwa wasafiri dhaifu na wachovu. Kwa kulinda kwa uangalifu, nafsi inazuiwa kujionesha kuwa na haki. Mazoea sahihi yanatengenezwa. Kuna utambuzi makini kuhusu haki za watu wengine. Imani itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa roho inashikilia usukani, na kuitawala kaya yote. Chini ya mvuto mtakatifu wa kaya kama hiyo, kanuni za udugu zilizowekwa katika Neno la Mungu zinatambuliwa kwa upana zaidi na kutiiwa. - Southern Watchman, Jan. 19, 1904.

     *MUNGU AKUBARIKI     UNAPOTAFAKARI*

Leave a Reply