Kesha la asubuhi: Kuchimba Ndani Zaidi Kwenye Machimbo

*KESHA LA ASUBUHI*

*JUMATATU APRILI 9, 2018*

*Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Matendo 17:11.*

?Ni sawa na sahihi kuisoma Biblia; lakini wajibu wako haukomei hapo; kwani inakupasa uchunguze kurasa zake wewe mwenyewe. Elimu ya Mungu haipasi ipatikane bila jitihada ya akili, bila maombi kwa ajili ya hekima ili upate kutenga nafaka ya kweli kutoka kwenye makapi ambayo watu na Shetani wamewasilisha mafundisho ya ile kweli visivyo. Shetani na muungano wake wa mawakala wa kibinadamu wamenuia kuchanganya makapi ya uongo na ngano ya ile kweli. Inatupasa tuchunguze kwa bidii hazina iliyofichwa na kutafuta hekima kutoka mbinguni ili tuweze kutenganisha uvumbuzi wa kibinadamu na maagizo ya Mungu.

? Roho Mtakatifu atamsaidia mtafutaji wa ukweli mkuu na wa thamani ambao unahusiana na mpango wa ukombozi. Ninawasisitizia wote ukweli kwamba kusoma Maandiko juu juu hakutoshi. Ni lazima tuchunguze na hii maana yake ni kutenda yale yote Neno linayomaanisha. Kama vile mchimbaji wa madini anavyochimbua ardhi ili kugundua mikanda yake ya dhahabu, wewe pia inakupasa uchunguze Neno la Mungu ili kupata hazina iliyofichika ambayo kwa muda mrefu Shetani amekuwa akitafuta kumficha mwanadamu. Bwana anasema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo” (Yohana 7:17).

? Neno la Mungu ni ukweli na nuru na yapasa liwe taa miguuni pako, kukuongoza katika kila hatua kwenye njia iendayo kwenye malango ya mji wa Mungu. Ni kwa sababu hii, Shetani amekuwa akiweka jitihada za hali ya juu kuzuia njia ambayo imewekwa kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana kuipitia. Haipasi uingie kwenye Biblia na dhana zako na kufanya mitazamo yako kuwa kiini ambacho kwa hicho ukweli yapasa uzungukie.

? Inakupasa uweke pembeni fikra zako kwenye mlango wa uchunguzi nawe ukiwa na moyo mnyenyekevu, nafsi iliyofichwa katika Kristo, na maombi ya dhati, inakupasa utafute hekima kutoka kwa Mungu. Inakupasa ujisikie kwamba ni lazima ujue mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, kwa sababu yanahusu ustawi wako binafsi, wa milele. Biblia ni mwongozo ambao kupitia kwa huo unaweza kujua njia ya kufikia uzima wa milele. Kupita mambo yote, inakupasa ujue mapenzi na njia za Bwana. – Fundamentals of Christian Education, uk. 307, 308.

*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*

Leave a Reply