Kesha la asubuhi: Kufanya Kazi Kupitia Vyombo Vinyenyekevu

            *KESHA LA ASUBUHI*

             _IJUMAA MEI 25, 2018_

     *Kufanya Kazi Kupitia Vyombo
                   Vinyenyekevu*  _Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. 1 Wakorintho 1:25._

? Mungu atatembea juu ya watu wenye nafasi duni katika jamii, watu ambao hawajafikia kuwa wasiojali miale angavu ya nuru kupitia katika kutafakuri kwa muda mrefu juu ya nuru ya ukweli, na kukataa kufanya maboresho au mwendelezo wo wote ndani yake. Wengi kama hao wataonekana wakikimbia hapa na pale, wakibidishwa na Roho Mtakatifu wa Mungu kupeleka nuru ile kwa wengine. Ukweli wa neno la Mungu, ni kama moto katika mifupa yao, ukiwajaza kwa tamaa kuu ya kutaka kuwaelimisha wale wanaokaa gizani.

? Wengi, hata miongoni mwa wasomi, sasa wanatangaza maneno ya Mungu. Watoto wanahimizwa na Roho kwenda mbele na kutangaza ujumbe kutoka mbinguni. Roho amemwagwa kwa ajili ya wote watakaosikia ushawishi wake, na, huku wakiacha taratibu zote za kibinadamu, kanuni zake za lazima na njia zake za uangalifu, watatangaza ukweli kwa nguvu ya uwezo wa Roho. Makundi mengi watapokea imani na kujiunga katika majeshi ya Bwana.

? Wengi wa wale ambao wanakiri kuwa wafuasi wa Bwana kwa sasa hawajisalimisha kwa uongozi wa Roho wake, lakini wanajaribu kumfunga lijamu Roho Mtakatifu, na kumwendesha kama wapendavyo. Wote walio kama hao ni lazima waache kujitosheleza kwao, na kujisalimisha wenyewe bila kubakiza cho chote kwa Bwana, ili apate kutenda mapenzi yake mema ndani yao na kupitia kwao.

? Mapigo saba ya mwisho yako karibu kushuka juu ya wasiotii. Wengi wameacha wito wa injili uende bila kusikiwa; wamepimwa na kujaribiwa; lakini vizuizi vikuu vimeonekana kutisha mbele ya uso wao, vikizuia mwendo wao wa kusonga mbele. Kupitia katika imani, ustahimilivu, na ujasiri, wengi watavishinda vikwazo hivi na kutembea kwenda katika nuru yenye utukufu. Karibu pasipo kutambua vikwazo vimesimamishwa katika njia nyembamba; mawe ya kujikwaa yamewekwa katika njia hii; vyote hivi vitasukumwa mbali. Kinga ambayo wachungaji wa uongo wameweka kuyazunguka makundi yao ya kondoo zitakuwa kama hakuna; maelfu watapiga hatua kwenda kwenye nuru, na kufanya kazi ya kuieneza nuru hii. - Review and Herald, July 23, 1895.

              *MUNGU AKUBARIKI
                  UNAPOTAFAKARI*

Leave a Reply