KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO
06 June 2018
_*KUSHIRIKIANA NA
NGUVU YA MUNGU.*_? *“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” (Matendo 1:8).*
✍?Mungu amekusudia kutoacha chochote kisifanyike ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwenye taabu za adui. Baada ya kupaa kwa Kristo, Roho Mtakatifu alikabidhiwa kwa mwanadamu ili awasaidie wote ambao wangependa kushirikiana Naye katika kuiumba upya na kuijenga upya tabia yake. Sehemu ya Roho Mtakatifu katika kazi hii imefasiliwa na Mwokozi wetu. Anasema, “Atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu” (Yohana 16:8). Roho Mtakatifu ni msadikishaji, na pia ni mtakasaji.
✍?Kwa vile hakuna anayeweza kutubu dhambi zake hadi pale anapokuwa amesadikishwa, ulazima wa kuungana na Roho katika kazi yetu ili kuwafikia walioanguka ni dhahiri. Vipaji vyetu vyote vya kibinadamu vitatumiwa bure isipokuwa kama tumeungana na mawakala wa mbinguni.
✍? Ni kupitia ukosefu wa maarifa ya kweli zihuishazo, na nguvu potofu ya uovu, ndiyo maana watu wamedhoofika kiasi hicho, wamezama katika vina vya1
auharibifu wa dhambi. Malaika na wanadamu hawana budi kutenda kazi kwa upatanifu ili kuifundisha kweli ya Mungu kwa wale wasioijua, ili wawekwe huru dhidi ya vifungo vya dhambi. Ni kweli pekee ndiyo iwawekayo wanadamu huru. Uhuru huu upatikanao kupitia maarifa ya neno la kweli, unapaswa kutangazwa kwa kila kiumbe.
??♂```Yesu Kristo, Mungu Mwenyewe, na malaika wa mbinguni wanavutiwa na kazi hii kuu na takatifu. Mwanadamu amepewa heshima iliyotukuka ya kudhihirisha tabia ya kiungu kwa kujihusisha pasipo ubinafsi katika jitihada za kumwokoa mdhambi kutoka kwenye shimo la uharibifu ambamo ametumbukia.
??♂ Kila mtu atakayejisalimisha ili aelimishwe na Roho Mtakatifu atatumiwa kwa ajili ya ufanikishaji wa kusudi hili lililoasisiwa na mbingu. Kristo ndiye kiongozi wa kanisa Lake, na itamtukuza zaidi pale ambapo kila kipengele cha kanisa hilo kitajihusisha katika kazi ya wokovu wa roho. Lakini watendakazi wa kibinadamu wanahitaji kuacha nafasi zaidi kwa ajili ya Roho Mtakatifu kufanya kazi, ili watumishi wafungamanishwe pamoja; na kusonga mbele katika nguvu ya kundi moja la askari. Hebu wote wakumbuke kwamba sisi tu “tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.” (1 Wakorintho 4:9).```
*MUNGU AWE NANYI MNAPOJIKABIDHI KWAKE*
Related