KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO
18 Apr 2018
*_KUTAKASWA kWA NJIA YA NENO_*
? *Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Yohana 17:17.*
✍?Mzigo wa ombi la Yesu ulikuwa kwamba wale waliomwamini Yeye waweze kulindwa dhidi ya uovu wa dunia na kutakaswa kwa njia ya ile kweli. Yeye huwa hatuachi katika hali ya kubuni kusiko na uhakika kama ukweli ni nini, bali huongezea, “Neno lako ndiyo kweli.”
✍? Neno la Mungu ni njia ambayo kwayo utakaso wetu ni lazima ukamilishwe. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu sana, kwamba tujifahamishe maelekezo matakatifu ya Biblia. Ni jambo la muhimu kwetu kuelewa maneno ya uzima kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali kufahamishwa kuhusu mpango wa wokovu.
✍?Hatutakuwa na udhuru ikiwa, kutokana na uzembe wetu wenyewe, hatutajua madai ya Neno la Mungu. Mungu ametupatia Neno lake, udhihirisho wa mapenzi yake naye amewaahidi Roho Mtakatifu wale wanaomwomba, ili awaongoze kwenye kweli yote; na kila nafsi ambayo kwa uaminifu inatamani kufanya mapenzi ya Mungu itayajua mafundisho.
✍?Dunia imejazwa na mafundisho ya uongo; na tusipochunguza Maandiko kwa ajili yetu wenyewe kwa makusudi, tutakubali makosa yake kana kwamba ndio ukweli, tutakubali mila zake na kudanganya mioyo yetu wenyewe.
✍? Mafundisho na desturi za dunia vinatofautiana na ukweli wa Mungu. Wale wanaokusudia kugeuka kutoka katika kuitumikia dunia ili wamtumikie Mungu watahitaji msaada wa kimbingu. Itawapasa kukaza nyuso zao kama chuma kuelekea Sayuni. Watahisi upinzani wa dunia, mwili na mwovu, nao itawapasa waende kinyume cha roho na mivuto ya dunia.
✍?Tangu nyakati Mwana wa Mungu alipokabiliana na chuki zisizo na sababu na majivuno na hali ya kutokuamini ya watu, hakujawa na badiliko katika mtazamo wa dunia kwa dini ya Yesu. Watumishi wa Kristo ni lazima wakutane na roho ile ile ya upinzani na shutuma na ni lazima kwenda “nje ya kambi, tukichukua shutumu lake” (Waebrania 13:13).
??♂```Utume wa Yesu ulidhihirishwa kwa miujiza ambayo haikuwa na mashaka. Mafundisho yake yaliwashangaza watu. Mafundisho yake hayakuwa lugha za kitaalamu zilizokinzana za waandishi, zilizokuwa zimejawa na imani za mafumbo, ambazo zilikuwa na mizigo ya mifumo ya kipuuzi na ulazimishaji usio na maana;
??♂ lakini ni mfumo wa ile kweli ambao ndio uliokutana na mahitaji ya moyo. Mafundisho yake yalikuwa wazi, bayana na yenye upana. Ukweli halisi aliousema ulikuwa na uwezo wa kusadikisha, nao ulivutia usikivu wa watu. – Review and Herald, Feb. 7, 1888.```
*MUNGU AWABARIKI NYOTE MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
Related