*KESHA LA ASUBUHI*
_JUMAPILI APRILI 29, 2018_
? Sauti ya Mungu inanena nasi kupitia katika Neno lake na zipo sauti nyingi tutakazozisikia; lakini Kristo amesema tuwe macho dhidi ya wale watakaosema, Kristo yupo hapa au Kristo yuko kule. Sasa, tutajuaje kwamba hawana ukweli, kama tusipoleta kila kitu kwenye Maandiko? Kristo ametuonya kuwa macho na manabii wa uongo ambao watatujia katika jina lake, wakisema kwamba wao ni Kristo.
? Sasa, ikiwa utakuwa katika mtazamo kwamba sio muhimu kwenu kuelewa Maandiko ninyi wenyewe, mtakuwa hatarini kupotezwa na mafundisho haya. Kristo amesema kwamba kutakuwa na kundi ambalo siku ile ya malipo hukumuni litasema, “Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Lakini Kristo atasema, “Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22, 23)…
? Muda unakuja ambapo Shetani atafanya miujiza mbele za macho yenu, akidai kwamba ndiye Kristo; na kama miguu yako siyo imara kwenye ukweli wa Mungu, utapelekwa mbali kutoka kwenye msingi wako. Usalama wako pekee ni kuchunguza ukweli ili kupata hazina zilizofichwa. Chimbua ukweli kama mtu achimbaye hazina ardhini nawe wasilisha Neno la Mungu, Biblia, mbele za Baba wa mbinguni, na kusema, Niangazie; nifundishe kile kilicho kweli.
? Roho wake Mtakatifu atakapowajia mioyoni mwenu, ili kuweka mguso wa ukweli nafsini mwenu, haitakuwa rahisi kwenu kuuachia. Mmepata uzoefu huo katika kuyachunguza Maandiko, kiasi kwamba kila sehemu imethibitishwa. Na ni muhimu kwamba mdumu kuchunguza Maandiko. Inakupasa uhifadhi Neno la Mungu moyoni; kwani mnaweza kutenganishwa na kuwekwa mahali ambapo hutakuwa na fursa nzuri ya kukutana na watoto wa Mungu. Hapo ndipo mtakapohitaji hazina za Neno la Mungu mioyoni mwenu na wakati upinzani utakapowajia ukiwazingira, mtahitaji kuleta kila kitu kwenye Maandiko. Review and Herald, Aprili 3, 1888.
*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*