Kesha la asubuhi: Kwenda kwenye chanzo cha Nuru

*KESHA,,, LA,, ASUBUHI "*

Jumatano. *04/04/2018*

*"Kwenda Kwenye Chanzo cha Nuru ?"*  ?...   ?

*"""Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. Zaburi 119:130."""* ✍??...Nyakati fulani imekuwa kwamba watu wenye uwezo mkubwa kiakili, walioendelea kielimu na kwa ustaarabu, hushindwa kuelewa aya fulani za Maandiko, wakati wale wengine ambao hawajafunzwa, hupata maana, wakipata nguvu na faraja katika kile ambacho walioelimika wanasema ni fumbo au kukiacha kama kisicho cha muhimu. Kwanini iwe hivi? Nimeelezwa kwamba kundi hili la wasio na elimu kubwa hawategemei ufahamu wao. Hawa huenda kwenye Chanzo cha nuru, Yeye ambaye ndiye aliyevuvia Maandiko na kwa unyenyekevu wa moyo humwomba Mungu hekima na huwa wanaipokea. Yapo machimbo ya ukweli ambayo bado hayajagunduliwa na mwenye kutafuta kwa dhati.

   ✍??......Kristo aliwakilisha ukweli kama hazina iliyofichwa shambani. Haikai juu tu kwenye uso wa nchi; ni lazima tuichimbue. Hata hivyo, mafanikio yetu katika kuipata, hayategemei sana uwezo wetu wa kiakili bali unyenyekevu wa moyo na imani inayoshikilia msaada wa Mungu.

 ✍??..Bila uongozi wa Roho Mtakatifu itaendelea kuwa rahisi kwetu kulazimisha Maandiko au kuyatafsiri vibaya. Upo usomaji mwingi wa Biblia usio na faida na mara nyingi hujeruhi kwa hakika. Pale Neno la Mungu linapofunguliwa bila kicho na wala ombi; wakati mawazo na matashi yasipoelekezwa kwa Mungu au katika upatanifu na mapenzi yake, moyo huwa katika giza la mashaka; na katika somo lile lile la Biblia, hali ya kuwa na shaka huimarika. Adui hutawala mawazo na hupendekeza fasiri zisizo sahihi.

✍??.....Wakati wowote watu wasipotafuta, kwa neno na kwa tendo, kuwa katika upatanifu na Mungu, hata wawe wameelimika kiasi gani, inawezekana sana kwa hao kukosea katika uelewa wa Maandiko na sio salama kutumainia maelezo yao. Tunapotaka kutenda mapenzi ya Mungu kweli, Roho Mtakatifu huchukua kanuni za Neno lake na kuzifanya kuwa kanuni za maisha, huku akiziandika kwenye bamba za moyo. Na ni wale tu wanaoifuata nuru ambayo imekwisha tolewa wanaoweza kutumaini kupokea nuru ya ziada ya Roho. – Testimonies, vol. 5, uk. 704, 705.

*”TAFAKARI,,, NJEMA,,, “*

Leave a Reply