Kesha la asubuhi: Tukiwa na vyombo vitupu

               KESHA LA ASUBUHI 

               ALHAMISI 12-04-2018

                     *TUKIWA NA*   
                   *VYOMBO VITUPU.* ? *Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. 2 Wakorintho 4:7.*

✍? _Swali hili limeulizwa, “Ni aina gani ya vyombo ambavyo Roho huvitumia?” Kristo anasema nini? – “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:28-30). Ni aina gani ya vyombo vinavyofaa kwa ajili ya matumizi yake Bwana? – Vyombo vitupu. Tunapotoa kila uchafu moyoni, tunakuwa tayari kutumiwa._

✍? _Je nafsi yetu tumeitoa? Je, tumeponywa kutokana na kupanga kibinafsi? Ah, natamani tungepunguza kuitumikia nafsi! Hebu Bwana asafishe watu wake, walimu na makanisa._ 

✍? _Yeye ametoa kanuni iwe mwongozo kwa wote na katika hii hapatakiwi kuwa na namna yoyote ya kuiacha njia kizembe. Lakini huwa kumekuwa, na bado hili lipo, hali ya kuyumba kutoka kwenye kanuni za haki. Hali hii ya mambo itadumu kwa muda gani? Bwana atawezaje kututumia kama vyombo kwa ajili ya utumishi mtakatifu tusipoondoa vyote ndani yetu wenyewe na kutoa nafasi kwa ajili ya ya utendakazi wa Roho wake?_

✍? _Mungu anawaita watu wake wamdhihirishe. Je, dunia itaonesha kanuni za uadilifu ambazo kanisa halishikilii? Tamaa binafsi za kuwa wa kwanza vitaendelea kuoneshwa na wafuasi wa Kristo? Kanuni zinazopendwa nao hazitawekwa kwenye msingi wa kweli, yaani Kristo Yesu? Ni vitu gani tutakavyoweka kwenye msingi, ili pasiendelee kuwa na uhasama, badala yake umoja, ndani ya kanisa?_

✍? _Tutaweka kwenye msingi mbao, nyasi kavu au mabua? Je, badala yake si tulete vitu vya thamani - dhahabu, fedha, vito vya thamani? Hatutatofautisha kwa namna iliyo dhahiri kabisa kati ya makapi na ngano? Hatutatambua kwamba ni lazima tupokee Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, kwamba anaweza kutuumba na kutengeneza maisha?_

```Tunaishi nyakati za hatari. Kwa kumuogopa Mungu naweza kusema kwamba ufafanuzi wa kweli wa Maandiko ni wa muhimu kwa ajili ya maendeleo sahihi ya kimaadili kwa ajili ya tabia zetu.```

```Mioyo na roho vinapokuwa vimefanyiwa kazi na Roho, nafsi inapokufa, ukweli una uwezo wa kudumu kupanuka na kuwa na maendeleo mapya. Ukweli unapoumba tabia zetu, utaonekana kuwa ukweli hasa. – Review and Herald, Feb. 28, 1899.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*

Leave a Reply