Kesha la asubuhi: UKARIMU

*KESHA LA ASUBUHI*

_JUMATANO MACHI 21, 2018_


*Ukarimu*
```Maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. 2 Wakorintho 8:2.```


? Ni pale tu makusudi ya Mkristo yanapotambulika kikamilifu na dhamiri inapoamshwa kwa ajili ya wajibu, ambapo nuru ya Mungu huweka mguso kwenye moyo na tabia, huo ubinafsi unashindwa na nia ya Kristo inadhihirishwa. Roho Mtakatifu, akifanya kazi mioyoni mwa watu na tabia zao, ataondolea mbali mielekeo yote ya tamaa, mielekeo ya kufanya mambo kwa udanganyifu.

? Mjumbe wa Bwana anapokuwa akiuleta ujumbe kanisani, Mungu ananena kwa watu, akiamsha dhamiri zao zione kwamba hawajaleta zaka kwa uaminifu kwa Bwana, na kwamba pale ambapo haikuonekana kuwa muda unaofaa kutoa, wameshindwa kumletea sadaka yao. Wametumia pesa iliyo mali ya Bwana kwa ajili yao wenyewe, katika kujenga majumba, katika kununua farasi, vyombo vya usafiri, au ardhi. Huwa wanafanya hili wakitumaini kupata mapato makubwa na kila mwaka udhuru wao ni huo huo. “Je, mwanadamu atamwibia Mungu?” (Malaki 3:8). Kwa kweli, amekuwa akilifanya hili mara nyingi, kwa sababu hajawa mtu wa kiroho, kuweza kuona mambo ya kiroho.

? Kwa wapenda dunia, wabinafsi, Bwana amekuwa akitenda nyakati fulani, kwa namna iliyo wazi kabisa. Akili zao ziliangazwa kwa Roho Mtakatifu, mioyo yao ikahisi mguso wake unaolainisha na kunyenyekeza. Kutokana na utambuzi wa wingi wa rehema na neema ya Mungu, walijisikia kuwa ni wajibu wao kuhimiza mpango wake, kuujenga ufalme wake. Walikumbuka sharti, “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi” (Mathayo 6:19, 20).

? Walijisikia kuwa na shauku ya kuwa na sehemu kwenye ufalme wa Mungu, nao wakaahidi kutoa pesa zao kwa ajili ya baadhi ya shughuli mbalimbali katika kazi ya Mungu. Ahadi hiyo haikutolewa kwa mwanadamu, bali kwa Mungu mbele za malaika zake, ambao walikuwa wakipita mioyoni mwa hawa watu wabinafsi, wapendao pesa. – Review and Herald, Mei 23, 1893.

*MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*

Leave a Reply