*KESHA LA ASUBUHI*
“`JUMAMOSI MACHI 24, 2018“`
*Umaridadi wa Nje*Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mithali 31:21, 22._
✍? Elimisha, elimisha, elimisha. Wazazi wanaopokea ile kweli yapasa wapatanishe mazoea na desturi zao na maelekezo ambayo Mungu ameyatoa. Ni shauku ya Mungu kwamba wote wakumbuke kwamba utumishi wa Mungu ni msafi na mtakatifu na kwamba wale wanaopokea ile kweli ni lazima wasafishwe katika mielekeo, tabia, mioyo, mazungumzo, katika mavazi, na nyumbani, ili malaika wa Mungu ambao hawawaoni, wapate kuja na kuhudumia wale watakaokuwa warithi wa wokovu.
✍? Wale wote wanaojiunga na kanisa sharti wadhihirishe badiliko la tabia inayoonesha kicho chao kwa mambo matakatifu. Sharti maisha yao yote yajengwe kulingana na uzuri wa Kristo Yesu. Wale wanaojiunga na kanisa yapasa wawe wanyenyekevu kiasi cha kutosha kupokea maelekezo katika maeneo ambayo hawajawa makini kwayo na ambayo wanaweza na ni lazima wabadilike katika hayo.
✍? Ni lazima waoneshe mvuto wa Kikristo. Wale wasiofanya mabadiliko katika maneno au mwenendo, katika namna yao ya kuvaa au katika nyumba zao, huwa wanaishi kwa ajili yao wenyewe na sio kwa ajili ya Kristo. Hawajaumbwa upya katika Kristo Yesu, hata kufikia usafi wa moyo na mazingira ya nje. Wakristo watatambuliwa kutokana na tunda wanalolionesha katika kazi ya matengenezo. Kila Mkristo wa kweli ataonesha kile ambacho ukweli wa injili umekifanya kwake. Yeye ambaye amefanywa kuwa mwana wa Mungu ni lazima awe na mazoea ya kutenda kwa unadhifu na usafi.
✍? Kila tendo, hata liwe dogo kiasi gani, lina mvuto wake. Bwana anatamani kumfanya kila mtu kuwa wakala ambaye kupitia kwake Kristo anaweza kudhihirisha Roho wake Mtakatifu. Kwa namna yoyote haipasi Wakristo wawe wazembe au wasiojali suala la mwonekano wao wa nje. Inapasa wawe maridadi, japo bila mapambo. Inapasa wawe wasafi ndani na nje. – Testimonies to Southern Africa, uk. 87.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI SOMO LA LEO*