Mambo kama haya ndio yamenifanya nichukue siasa kwani ili uwe mwanasiasa lazima uwe muongo na upungukiwe na ubinadamu kidogo! Usichanganye, nimeongolea “siasa” sio “uongozi”! Kuna tofauti ya viongozi na wana siasa. Tatizo la Africa haswa Tanzania kuwa kiongozi unajikuta unalazimika kupitia siasa! Tuna baadhi ya viongozi wazuri sana ila wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwani kila kitu kinahusishwa na siasa! Mbaya zaidi ni pale siasa inapo ingizwa kwenye mambo ambayo yanahatarisha uhai wa binadamu na watu wanaona ni sawa!! Katuroga nani sisi?! ……..Mimi nasema imefika wakati wa wanawake kuongoza ngazi zote hadi urais kwani hawa wanaume wana roho za paka!! Just unbelievable!!! “Nyufa kwenye hosteli za UDSM: Wahandisi na wataalamu wengine wa majengo wafanye ukaguzi na kuchukua hatua stahiki. Ni vyema hili jambo lisichukuliwe kisiasa. ” Mhe ShyRose Bhanji