Kuna watu hujishusha thamani wanapoangalia wengine wanaoonekana wamewazidi nafasi bila kujua wao huenda ni MUHIMU kuliko hata wanaowaangalia sababu ndio wanaowasababishia UKAMILIFU,
Natamani ujue kitu kimoja hapo ulipo iwe wewe ni Mpishi, housegirl, shamba boy, messenger ama mwajiriwa tu wa ofisi fulani, thamini na RINGIA unachokifanya na usiruhusu mtu akudharau, hiko unachokifanya Boss wako hata awe na mamilioni bado hawezi kufanya na hiyo ni NGUVU. Ukichukua muda kuchunguza utagundua hakuna alie muhimu zaidi ya mwingine na KILA MTU NI MUHIMU, vipi leo mahousegirl wakigoma wote hata thamani ya hela yako utaiona!?
Wamama wangapi nyumba zitawashinda, Jiulize Unaweza kufanya wanachokifanya wao fully!? Maana unaitwa Boss sababu kuna watu WALIOKUBALI kukutumikia, Ama hata Kama una ofisi wafanyakazi wakaondoka wote unaweza kufanya kwa ufanisi hiko wanachokifanya wao!?? Kitendo chochote cha kuweza kufanya asichoweza mwingine ni UPEKEE, na upekee ni NGUVU haijalishi unachokifanya ni kitu gani, hivyo usijidharau wala kuona kuna wanaostahili na wasiostahili.. hata kama we ni mpika maandazi mazuri mtaani RINGA, usijidharau halafu ukamuheshimu mama anaepaki gari kila siku kununua maandazi yako kwa kuhisi yeye ndio bora hapana, yeye hawezi kupika kama wewe ndiomana anapaki kwako, na huo uliopewa ni upekee mkubwa ambao wewe ndio wa kuamua uutumie vipi ili uwe na faida sababu hakuna mwingine anaepika kama wewe,
MUNGU AMEKUPA NGUVU YAKO KUBWA kwa kukutunukia uwezo wa tofauti, hakuna alie BORA zaidi ya mwengine ila tuna MAJAALIWA TOFAUTI, asiekuwa na hiki unakuta ana kingine and viceversa, hivyo heshimu ulichonacho na UJITHAMINI, na zaidi tafuta njia ya kukifanya kwa UKUBWA hata kama ni kitu kidogo kiasi gani maana ndicho ulichopewa na MUNGU!! penye upekee wako ndipo UTAJIRI ULIPO. Haina maana kwakuwa UNATUMWA ukahisi wewe sio muhimu ama anaekutuma ndio mtu hapana, haijalishi unachokifanya ni nini since unaemfanyia hawezi kukifanya mwenyewe basi jua wewe ni wa muhimu pia.
Related