Stellah Gellan(kushoto) Yasinta (wapili kushoto), mwalimu wetu kipenzi Mr Casmir Nkuba aliambatana na mwanaye Aneth Nkuba (mtu kati) pamoja na Christian. Dhumuni la kukutana ilikuwa ni kumsalimia na kumkabidhi Ile zawadi ya Powerbank. Wapendwa wasomaji wangu, hawa ni baadhi tu ya wanafunzi wenzangu ambao ni wanafunzi waanzilishi wa Kowak Girls Secondary school, wakiwa pamoja na Mwalimu wetu ambaye alikuwa tukimuona ??? Alikuja kufundisha Kowak Girls akiwa kijana sana fresh from school. Ndo maana amekuwa karibu sana nasi wote. He’s such a good friend to all of us. Often nikiwa Bongoland huwa ndo mtu na socialize naye as ni mtu wa story sana. Kama wewe ni mtembeleaji wa hii blog basi utakuwa umeshawahi ona sura yake……… Kowak ilikuwa secondary ambayo nilianzia (Kowak ni kijijini kwa mama yangu mzazi. Ndipo alipo zaliwa) then nikamalizia Nurulyakini Secondary school iliyopo Temeke Mikoroshini. Nimefurahi sana kuona wanafunzi wenzangu baada ya miaka mingi sana. Class of 1995Haya hiyo ndo zawadi ya Powerbank, japo sijaelewa bado ni kitu gani lakini naona mwenyewe kafurahia. “Leo nimepata wageni ofisini kwangu, nao ni hao wanaonekana katika pichaa zilizorushwa hapa na Yasinta. Wageni hawa wameniletea zawadi nzuuuuri ya Powerbank ambayo ninyi nyote humu mmeamua kuninnunulia. Jamani ASANTENI SANA, Mwenyezi Mungu AWABARIKI wote. Awajalie Afya Njema pamoja na familia zenu. Awajalie mafanikio maradufu katika kazi zenu, pale mlipotoa kwa ajili yangu papokee zaidi. Kwa Powerbank hii nitahakikisha nakuwa online throughout” maneno yake Mwl. Casmir Nkuba Ladies, this was really nice. Thank you so much kwa kutuwakilisha. Mbarikiwe sana……..class of 1995 Rocks!
nawaalika kwenye sherehe ya jubilei ya miaka 25 ya shule yenu kowak girls itakayofanyika tarehe 26 august mwaka huu 2017 tafadhali mjulishe na mwingine. mawasiliano tazama hapo chini.