Leo naona watu wengi wamempongeza Diamond kwa kitendo cha kuonyesha kuunga mkono kazi za Harmonolize a.k.a KondeBoy. Diamond ameandika ujumbe mzuri sana ambao wengi wameamini unatoka moyoni! Hata mimi naamini umetoka moyoni mwake ?? embu usome ????
Kweli hata mimi nampongeza Diamond kwa kuweka his “ego down” na kuonyesha upendo kwa mwanamuziki ambaye yeye mwenyewe alisaidia makuzi yake wakati yupo WCB! Nikitendo kizuri sana na chakufurahisha, lakini nimeshindwa ku-ignore the odds! Au wengine wanaweza sema the ‘hidden agenda’ au ‘the motive behind’!
Kama utakua ulisoma post yangu nilio andika mwanzoni mwa wiki hii inayo isha yenye kichwa cha habari kisemacho “Wema Sepetu ni mwanamke dhahifu sana” basi utakua ulisoma kile kipengele ambacho nilisema Diamond anapenda sana ‘attention’ na hiyo ilikua moja ya sababu hakuweza kumualika Wema Sepetu kwenye sherehe za miaka 10 ya muziki wake. Sasa basi, tumia maneno yangu hayo kutafakari alichofanya Diamond siku ya leo!
Yes, Diamond amefanya vizuri kuandika juu ya kum-support Harmonize! Lakini ilikua lazima afanye leo hii ambapo Harmonize amepamba kurasa za magazeti na social media?! Absolutely Not! Again, kama ilivyokuwa kwa Wema Sepetu asingependa kuona anapata attention zaidi yake basi ndivyo ilivyokuwa kwa Harmonize leo! Diamond baada ya kuona it’s all about Harmonize akaona njia pekee ya kuivunja nguvu hii ya attention anayopewa Harmonize ni kufanya kitendo ambacho kitagusa hisia ya kila mtu na kuelekeza attention yote kwake katika njia iliyo salama bila watu kugundua his agenda! The only way to steal Harmonize’s moment was to take his ego down! And yes, he won! Nilikwambieni Diamond ni manipulator and narcissist, mtu mwenye hulka kama hizi ni wakuogopa sana kwasababu yupo teyari kufanya kitu chochote kile ili abaki kuwa on top!
Kama kweli Diamond angekua muungwana, na kweli nia yake ilikua ni njema basi angesubiri hii momentum iwe all about Harmonize! Angesubiri ipite angala hata kwa siku moja halafu akaonyesha ukarimu wake! Lakini kwasababu hilo alikua lengo lake ndio maana hakuweza kuvumilia! Na hii naona ni style ya Management yake! Mnakumbuka walivyo fanya kwenye ufunguzi wa EP ya Tanasha?! Walikua wanajua kabisa Diamond hato kaa kwenye ile event lakini wakawa wanacheza na hisia za Tanasha bila yeye kujua na watu kufikiria kama kuna kitu nyuma ya pazia! Yaliyotokea wote mnayajua, wakatengeneza tukio la “dharura” na kulitangaza dakika za mwisho kabisa akijua watu wameweka macho yao wakisubiria kumuona Diamond na timu yake inaingia ukumbini! Hii yote ilikua ni kuvunja nguvu ya attention kwa tukio la Tanasha na kuhamia kwake! Hii ni typical behavior ya mtu anayependa ku control watu kama property yake binafsi! Hii nikuonyesha kua I’m still in control of you and everything!
Anafanya hivi kupata attention na trust kwenye macho ya jamii (haswa kwa watu wasiopenda kufanya tafakari ya kina) wakati anajua kabisa kitendo hicho kitamkwanza au muumiza hisia za muhusika! Yani hapo huwenda Harmonize anasema seriously bro?! This was my moment why steal it from me?! Kweli kabisa Harmonize anaweza hasiseme hadharani jinsi Diamond alivyo mkwaza na kitendo hicho lakini nina huwakika kwa wale watu wake wakaribu anao waamini lazima atakua anasema hata wao watakua wameumizwa sana! Harmonize nakushauri be a bigger person! Usimuonyeshe kua umechukia, wewe mshukuru tu halafu endelea na maisha yako! Kwasababu usipo sema neno la kumshukuru utakua unampa more attention na kuharibu image yako mbele za watu! Huna haja ya kuandika kwenye social medias, mtumie private msg. Na watu wakikuuliza sema nimeshukuru basi! Waswahili wanasema “funika kombe mwanaharamu apite”!
Nawashangaa sana watu wanaosema eti hii inaonyesha jinsi Diamond alivyo komaa?! ?? You people must be out of your mind! Diamond, he is a very insecure person! Ndio maana hawezi ku consider hisia za mtu mwingine! Diamond his self esteem ni sawa na ZERO!! Ndio maana “kiki” is the only way for him to boost his esteem!! Mtu asiyejiamini ndio huwa saa zote yupo kwenye mood ya mashindano yasio na tija, wabongo wanasema “anapenda ligi”. Mimi katika masomo yangu ya Ethics kuna somo nilisoma linaitwa “Human being behavior” hivyo najua mtu mwenye kujiamini anafananaje! Diamond ni entertainer mzuri sana lakini ni manipulator na narcissist, mwenye very-very low self esteem!.
Anyway, mie yangu ni hayo tu! Nawatakieni wote mafanikio mema na wazidi kuipeperusha bendera yetu vizuri! Na hongera sana Harmonize kwa event nzuri.