Hii ni kwa wana Diaspora wenzangu tu wengine someni halafu mpite kimya! Kabla hamjaweka miguu yenu barabarani kwenda huko mnako kwenda naomba kwanza uhakiki uraia wako. Je, wewe bado ni Mtanzania au ulisha ukana uraia wako? Kumbuka Tanzania haina Dual citizenship! Na kama bado wewe ni raia wa Tanzania je, umeshaagana na ndugu zako kwamba hata kama hamta onana tena basi iwe hivyo na kuwa ni salama rohoni mwako?! Maana unaweza usiwaone tena, siyo kwasababu ya kifo hapana, kwasababu huwezi kukanyaga ardhi ya Tanzania!Kwanini nimesema haya niliyo yasema, ni kwasababu ninaona dalili za baadhi ya watu kuja kufutiwa haki yao ya kuzaliwa kama Mtanzania (uraia wao kufutwa kabisa) na wengine ambao walisha ukana Utanzania wanaweza kuwekewa "Red flag" na wasiruhusiwe kukanyaga Tanzania for a very long time! Sounds like a joke, huh! Wrong! This is not a joke so kindly take it very seriously!! Kumbuka ofisi ya Rais ni tasisi inayo jitegemea ambayo inauwezo na mamlaka ya kufanya hivyo pale watakapokuwa na sababu tosha kufanya hivyo!
Vile vile kumbuka kuwa Rais ndio mtu peke anaweka signature kwenye Hati Miliki ya viwanja na pia anauwezo wa kuifuta na kuweka majina ya wamiliki wapya, hivyo kua muangalifu na maamuzi yako. Ukitaka kupambana na serikali lazima uwe umejipanga uwe na plan A to Z! Siyo plan A, B, sijui na C hapana! Uwe na plan zooote intact!! Nimewatolea siri tusije laumiana huko mbele ? Otherwise, nawatakieni matembezi mema kwa wale mtakao kwenda matembezi ? #NotWorthIt
Related