Je, umeshawahi kukutwa na hali kama hii? Hali ya kujishusha zaidi ya mtoto ili tu uweze kuwa na mtu au watu fulani katika maisha yako? Hali ya kujishusha thamani yako na saa nyingine kupoteza utu wako ili tu fulani au kundi fulani likupende? (comprising your morals and values, loosing who you are for the sake of afraiding being alone). Kuna wengine mpaka wana acha kupigania ndoto zao kwasababu wanaona watapoteza baadhi ya watu katika maisha yao. Wengine wanaishi maisha ambayo siyo ya hualisia ili tu kuwafurahisha watu fulani ili waendelee kua kwenye maisha yao! Nikitu kibaya sana kama unaweza kupoteza nguvu uliyonayo ndani yako ambayo umepewa na Mungu eti kwasababu ya kutaka kukubalika na watu fulani au kwasababu unaogopa kutembea mwenyewe kwenye maishai yako. Duniani hapa kila mmoja amepangiwa safari yake na Mwenyezi Mungu, na wengine huwenda tumepangiwa safari zetu kuwa tutembee wenyewe sasa basi ukiona kama unapoteza hualisia wako na utu wako kwasababu ya kitu au mtu fulani au watu fulani, basi jua kua safari yako umepangiwa kutembea mwenyewe! Don't ever sacrifice your happiness, morals, values, dignity, humanity kwasababu tu yakuogopa kutembea mwenyewe. Majasiri siku zote wanatembea wenyewe! Wanaweza wakachukua muda mrefu kufika lakini atafika akiwa salama na kwa ujasiri. Usiogope! Maana lazima kunawakati utafika itabidi tu uwe mwenyewe, anza sasa kabla hujachelewa ukaja sema "laiti ningelijua"! Usilazimishe mambo! Anza safari mengine muachie Mungu!