Nimependa sana hizi picha za rafiki yangu wa miaka mingi sana toka tupo shule pale Kowak Girls Secondary school iliyopo wilaya ya Rorya, mkowa wa Mara. Hapo ndipo tulikutana na mpaka leo hii zaidi ya miaka 20 bado tu marafiki sana. Yeye anaishi Geita………..ha! ha! ha! Ngoja niwape story moja hivi ya huyu rafiki yangu ??? kwa mara ya kwanza kusikia mvua inapiga kelele kwenye bati ilikuwa shuleni Kowak! Aliliaje sasa, alikuwa anatetemeka kama mtu mwenye mapepo! Tulikuwa wageni kabisa shule tupo form one akasema hakuwahi kusikia mvua ikifanya hivyo , tukawa tunamshangaa lol! Kumbe toka azaliwe amekulia kwenye nyumba za ghorofa ??marehemu baba yake alikuwa General Manager wa Mwatex hivyo siku zote ameishi kwenye nyumba za shirika. Halafu shule alisoma Nyakaoja, Mwanza ambapo nazo ni ghorofa. Maisha ya watu na experience ni tofauti sana, kile ambacho wewe unaweza kufikiria kuwa ni kitu cha kawaida “normal /simple thing” kumbe kwa mwingine ni miujiza! Lakini bado wote ni binadamu na thamani yetu wote ni sawa kabisa…………Kuna binamu yangu yeye alikuwa anasema anaomba Mungu amjalie apate elimu nzuri na pesa ya kuweza kumjengea mama yake nyumba yenye paa ya “mabati” eti naye aweze sikia sauti ya mvua ikinyesha kama wengine ?? kwani akiwa ndani ya nyumba ya “majani” hasikii wala hajui mvua kama inanyesha mpaka atoke nje!! Lakini Mungu si Athumani, her wishes came true! Nasasa hivi ni judge mwenye PhD naalipo anza kazi kitu cha kwanza alimjengea mama yake nyumba ya “mabati”!??Prisca umependeza sana. Mbarikiwe wewe na familia yako. Much love
Hahaaaaa umenikumbusha mvua za mawe kowak my dear ubarikiwe na mungu aendelee kutuweka