Regrann from @mutwiba - MJADALA
Kwa wale wenye uelewa wa maswali yajayo naomba tusaidiane kuyatafakari na naamini tutapata majibu ama maswali zaidi yatakayohitaji ama kuleta majibu zaidi. Kwenye hili la Makonda na 'watelekezwa' nimejiuliza baadhi ya maswali. Na kwa kuwa penye wengi haliharibiki neno, wacha niulize hapa ili ukiweza jibu lolote kati ya maswali haya.
MJADALA WA HESHIMA UTATHAMINIWA
1: Hili la wanawake kutelekezwa na watoto wao linatokea Dar tu ama hata mikoani lipo?
2: Wanaotajwa Dar wakikimbilia mikoani ambako mpango ama mkakati huu haupo, watasakwa ama? Na watakaotajwa kwa chuki na kuharibiwa mahusiano yao ya sasa watafidiwa?
3: Hili la kuwataja wanaume wanaoaminika kutelekeza watoto linatendeka kisheria ama ni ubunifu wa mkuu wa mkoa? Kama ni kwa mujibu wa sheria, si lifanyike nchi nzima? Kama ni ubunifu wa Mkuu wa Mkoa, akiacha ama kuachishwa kazi na ubunifu wake usio katika maandiko unakuwa umefia hapo?
4: Hudhani kwamba ingekuwa vema kuandaa workshop ama hata matangazo ya radio ya kuwafunza sheria za ndoa / mahusiano wanawake waliotelekezwa na wanaotaka kuingia kwenye mahusiano?
5: Mhe. Mkuu wa Mkoa akishakutana nao, wakishawataja watu waliowatelekeza, atawatatulia tatizo lao ama atawaelekeza Mahakamani ambako sheria ambazo zipo tayari zinastahili kuchukua mkondo wake?
6: kilichoonekana juzi ni kipi? (i) wanawake waliotelekezwa? (ii) wanaume waliotelekeza? (iii) mfumo wa sheria usiotenda haki kwa wanawake? (iv) wanawake wasiojua haki zao ambazo walistahili kuzisaka na kuzipata kabla ya kumfikia Mkuu wa Mkoa?
Yaani kilichodhihirika leo ni jambo la kuihurumia jamii yetu kwa kutojua ama kupuuza sheria
Na kwa kuwa na imani katika njia isiyotufikisha tunakotakiwa kwenda.
My two cents.
Na natunza haki ya kukosea na kukosolewa.
Mzee wa Changamoto - #regrann
Related