“….labda ningekuwa naanza maisha leo ningerudi mfumo wa wazazi………hawa watoto ndio maisha yangu…….pia katika uzima ni parterns wakudumu”~~~~ Dr Lennard Tenende
Haya msikilize mzee wetu Dr. Lennard Tenende akielezea historia ya maisha yake. Naona ni mzee mwenye uzoefu mzuri sana katika mambo mbali mbali ya taaluma na kijamii. Msikilize mwenyewe.
Kumbe mzee Tenende ndio muanzilishi wa DICOTA?! Mmh! Mimi sio mpenzi wa DICOTA, maybe I need more education about DICOTA lakini niliwahi kumuuliza "Dr Ndaga" alipokuwa President wa DICOTA akasema "ni chama cha Educated Elite" ambao wanafanya mambo "makubwa makubwa" sio kuandaa BBQ na baby-shower parties!! Sasa mimi I don't consider myself "educate" or "elite" hivyo siwezi kujihusisha na DICOTA. Plus inawezekana DICOTA ina nia na malengo mazuri lakini naamini kuna watu fulani wameingia kwenye uongozi wa DICOTA ambao hawana nia nzuri na wataivuruga sana hiyo DICOTA! Kama mnaweza kuwatoa muwatoe. Lakini hayo ni maoni yangu tu, you can ignore me as I'm not a part of "Educated Elite" ??? So funny!.......?? Btw, wale walio wasema Bungeni ni wanachama wa Chadema sio mimi naomba ieleweke hivyo.
"Ni kati ya achievement ni kubwa kuliko hayo ma-PhD unayo yasema"! Hayo ni maneno yake mzee Dr Lennard Tenende kuhusu mkewe. Wow! What a humble man! Yani mwingine angekazana kusifia hayo ma-PhD yake wee mpaka mngekoma, Wahaya mpo? ?? Dr. Mwakasisi umemsikia mwenzako ?? ............. Halafu nyie wadada wa 21st century mnaona wazee wetu walikuwa hawaangalii kama umepaka poda, wewe kwenye mchaka mchaka akaona mdada mrembo wa kuoa! Sasa nyie poda mnapaka na editing juu halafu ndoa baada ya miezi 6 imekwisha ?? Stop being so fake, let the man fall in love with your heart and character not your makeup and lipstick ??............... Nimeona. Mzee Tenende amekuwa emotional kidogo kuhusu kuwa na watoto wengi, amesema kitu ambacho Vivica Fox alisema kwa Oprah (SomaHapa) kuwa anajutia kutokuwa na watoto, kama angelijua angezaa hata watano! It really got me thinking ??....... nice interview!