Wapendwa wasomaji wangu, hapa tupo kwa ajili ya kufunzana, kufurahi, na kucheka. Na pale inapokuwa ngumu kufanya hivyo kwasababu ya mitihani ya dunia hii basi tutafarijiana na kupeana moyo…….Basi miaka 7 ilivyo pita, siku ya tarehe 2 mwezi wa 7, mmoja ya wadau wangu (nimemuita “mdau” kwasababu huwa natumiaga picha zake na za familia yake hapa kwa hii blog bila tatizo lolote) alipatwa na msiba wa baba yake mzazi. Hivyo imekuwa ni taratibu ya familia yao kufanya ibada ya kukumbuka mpendwa wao kulingana na imani ya dini yao na mila zao. Kwa kawaida huwa wanaenda kwenye kaburi la baba yao na kusafisha kama picha zinavyo onekana hapo chini! ?…….. Kwakweli siwezi wadanganya mimi binafsi ndio kwa mara ya kwanza kuona ibada hii inavyo fanywa (japo nikwenye picha). Huwa nasikia watu wakisema walienda kusafisha kaburi lakini sikuwahi shuhudia wala kuona kwa picha. Hivyo nimejifunza kitu hapa!….. Naomba usinicheke au kunishangaa ila elewa yakwamba mimi ni Msabato na kwenye ukoo wetu wengi ni Wasabato hivyo ibada kama hizi huwa hatuzifanyi kwani Wasabato hatuamini katika ibada baada ya kifo!…… Naona hata aibu kusema, lakini hali halisi ya yale makaburi ya kwetu Utegi ni pori hata nyoka nadhani wanaishi humo ??? upande wa mama yangu wao ni Roman Catholic hivyo mama zangu wakubwa na wajomba zangu ndo huwa nasikia wakienda safisha makaburi. Mama yangu alibadili dhehebu yeye ni Msabato hivyo huwa ashiriki ibada hizo ?? …… anyway nimejifunza kitu kuwa siyo lazima kufanya ibada kama wengine bali unaweza kupatengeneza pawe pasafi just for the dignity. Enyi Wasabato wa Bongoland msije nitoa roho ??? Wasabato wenzetu wa huku makaburi yao masafi kuna watu wanasafisha kila siku. Sasa nyie vipi bwana ?? acheni hizo ??
Ok hivi ndivyo Foster alianza siku yake. Kwa kuweka status hii kwenye Facebook account yak. Very touchy!……Kaburi la marehemu mzee Joseph Stanley Mbuna kama linavyo onekana Mama, mke wa marehemu ambaye pia ni mama mzazi wa Foster na bibi yake the Upcoming stylish Nathaniel (mchungulie hapa)
Foster akiwa na mama yake Mrs. MbunaKazi ya kusafisha ikiendelea…..ukimtegemea Mungu hata kwenye huzuni na maumivu makali utapata nguvu!Foster na mdogo wakeFoster na wadogo wakeFoster na mdogo wake pamoja na wanawe Foster akipozi kwenye kaburi la babaMama Foster na wanawe Uncle and nephewsWapendwa, poleni sana kwa msiba wa baba. Mungu wa Mbinguni azidi wapa faraja kwa kutegemea yeye pekee kuwa yeye tu atosha! Upendo, amani, na mshikamano vikadumu siku zote katika familia yenu!……… Bwana alito, na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote……. Azidi kupumzika katika amani ya Bwana marehemu mzee Joseph Stanley Mbuna !
NOTE: Picha zote kwahisani ya E.P.M photography. Kwa mahitaji yako ya picha tafadhali usisite kuwatafuta. Kazi yao ni nzuri na matokeo utayapenda!