Part 1. My late dad- in yellow and white. Mimi one of the little girls namwangalia babangu! . . Leo ni miaka 13 toka baba yetu atuache..??? Sitokaaa kuisahau siku ya Jumanne September 21 2004. Ilikuwa mida ya Sasa 1 usiku nikiwa mabibo hostel nilipigiwa simu na classmates wangu wa kiume @Gesona, Jerry Kajiru na wengine wakiniuliza nipo wapi wanataka twende sehemu nje ya mabibo hostel tukale chakula. Nikawaambia nipo block F basi wakanifata wakasema hiyo bar iko mbezi beach.Hao tukaondoka tukiwa njiani kuelekea huko nikapigiwa simu na Fideline Iranga, akiniuliza Mange uko wapi? Nikamwambia nipo njiani na washkaji tunaenda kula, akaniuliza ni kina nani? Nkamjibu huwajui, akawa very interested kujua niko na kina nani na tunaenda wapi mpaka nikastuka kidogo..Sjakaaa dakika 2 nikapigiwa simu na Carolyne Machange (Marehemu pia) akaniuliza Mange uko wapi? Mama yanguuuu nilitupa simu nkaaanza kuliaaaaaa sijui nalia nini?? Ila nilijua kuna tatizo kubwa na hakuna anaeweza kuniambia. Nikaannza kuwauliza washkjaji niliokuwa nao kwenye gari Jamani niambieni kuna nini? Something is wrong ? Wanajifanya kunishangaaa wananiuliza mange Unalia nini? Mbona hatukuelewi?? Nikawauliza Jamani mbona tunaenda Mbezi beach? Toka lini tunaenda kula mbali hivyo? Na huko ndo kwetu. Out of nowhere nilianza kuscream 'God Please not my dad' sijui why ila nilihisi ni babangu sababu watu wasingehangaika kunicheki vile Kama isingekuwa babangu coz wanajua nilikuwaje na babangu. Hapo rafiki zangu wananinyang'anya simu ili mtu mwingine asinipigie. Nalia kilio bila kujua nalilia nini. Nkachukua simu nkadial namba ya babangu ikawa imezimwa, mama yangu nikaanza kupiga mayoweeeeeeeeeeee why namba ya babangu imezimwa... gari ilivyoanza kuelekea kwetu nawauliza rafiki zangu mbona mnanipeleka nyumbani jamani?? Huku naliaaaa, wako kimya hawana jibu. . . Nakumbuka kama ilikuwa jana, tulivyofika kwetu mlinzi akaja kufungua geti nikawa namuuliza 'Babu kuna nini babu' Babu anaangalia chini, Hanijibu ile tunaingia nikaona gari ya babangu imepaki kidogo nkapata hope labda sio baba maana kama gari yake ipo it's means hajapata car accident na hawezi kufa kwa njia yoyote ile ingine sababu alikuwa mzima kabisaaa. Part 2. My dad (Mkandarasi) akikabidhi either College ya Veta au barabara (sikumbuki vizuri) kwa Mkapa . . . Basi nikashuka kwenye gari nakumbuka mtu wa kwanza kumuona alikuwa houseboy wetu Kaka Kibesa(marehemu pia) alikuwa houseboy wetu wa watangia Mimi sijazaliwa, aliletwaga na mama yangu mzazi kutoka Lindi, mmakonde mwenzie. Hata mama yangu alivyoachika Kaka Kibesa alibaki na aliendelea kunilea na alitulea watoto wote.R.I.P Kaka Kibesa. Kwa kumwangalia usoni tu nilijua ni baba, he looked so broken, nikamuuliza Kaka Kibesa naomba uniambie kuna nini, hakujibu kitu zaidi ya 'Panda juu Mange' . . Naingia ndani nakuta tayari kuna Watu wachache wamekaaa kwenye mikeka wanalia, mama yangu nilidataaaaaaa. Nilipanda zile ngazi kwenda upstairs Kama kichaaaaaaaaa, kuingia chumbani kwa baba na mama namuona step mom wangu kitandani analia huku watu wanambeleza, Mungu wangu nilianza kukaaaa chini na kusimama, najitupa nainuka , tumbo linaniuma, nilipata period hapo hapo, pale ndo nilipojua baba yangu kafariki. That was a defining moment.Nakumbuka sentensi ya kwanza nilisema ilikuwa ' Hakuna Mungu jamani, kungekuwa na Mungu asingemchukua babangu jamani' nikaanza kuuliza kafaje wakati gari yake ipo chini?? Hapo ndo nikaelezwa kajiua..... Dah sikuamini kajiua?? Ila it made sense!! . . Mara Kaka Kibesa akanitafa akanikabidhi barua aliyoniachia baba. Nkamuuliza aliacha barua ngapi akasema nne! Yangu, ya mke mkubwa, mke mdogo na ya kaka yake mkubwa!! Mikono ilikuwa inatetemeka kuifungua barua. Sikujua kama nilitaka kujua alichokiandika... Niliondoka nilipokua nimezungukwa na Watu nkajifungia nkaanza kuisoma. Like the true father that he was alikuwa kaniachia maagizo ya wapi ntapata pesa za school fees na matumizi mpaka Mirathi ikiwa settled! Na kuniagiza niwaangalie wadogo zangu. Nakumbuka sentensi ya kwanza ilikuwa ' Mwanangu Mange, utakapoipata Barua hiii nitakuwa nimeshatangulia mbele ya haki' Uwiii Barua ilijaaa machoziii. Wala hakugusia why kajiua Ila ni sababu alijua Mimi out of all people najua Sababu gani kajiua ?? Part 3. Msiba wa babangu ulikuwa kama movie kwangu. . . Baada ya hapo ilikuwa ni 2 long days za kuwasubiri wadogo zangu wa kiume waliokuwa wanasoma Kamuzu Academy-Malawi wafike nyumbani.nilikuwa nawawaza wao watahandle vipi situation sababu walikuwa wadogo.Nakumbuka sikuweza kutia kitu mdomoni toka nimeambiwa baba kafariki sababu nilihitaji kuwaona kaka zangu kwanza!Nakumbuka wadogo zangu walivyofika nilisikia tu vilio vimezidi nje. Niliwakimbilia nilihisi kama Baba anarudi.Tulihagiana wote wanne, Mimi, Step mom wangu,na wadogo zangu for the longest time. Na Nakumbuka ndogo wangu anaenifata alitake control of the situation mara moja, Yani alijua Sasa baba kaondoka lazma atake control. Alitukumbatia woooote akasema 'guys we will be okay' I swear hiyo sentensi ilinipa ahueni kubwa mnooo. Aliirudia ile sentensi kama mara 10 , ' We will be okay'. 30 mins later tulikaaa pamoja tukala chakula.?? . . Kifo cha babangu kinanisumbua mpaka Leo sababu I feel responsible somehow. I feel like I could have done something. I could have gotten him help. Baba yangu alikuwa ananitoa chuo kila siku anaiita ofisini kwake ananilalamikia about one thing and one person only.One of the 2 people aliemcause my father so much hurt ni Sumaye ndo maana mmeona issue yake ya kunyang'anywa Mashamba sikutaka kuposti.That time Sumaye alikuwa waziri mkuu. Labda Sumai hakufikiria kuwa threats alizomfanyia babangu kupitia mke mdogo na mali walizomfilisi yeye na mke mdogo zingeifikisha familia yetu hapo. Ntaishia hapo sababu nikiendelea itabidi nitaje na majina, kaka zangu hawatakagi niongeee hii issuie.Ila mke mdogo huwa siongei nae mpaka kesho. Nikimwonaga naskiaga roho inataka kunitoka? . . . Babangu aliondoka Kigoma 6 months before his death project ikiwa na matatizo na Sumaye akiwa anamwambia government haitomalizia malipo na ahand-in project ikiwa complete la sivyo anamfunga. Na hatokaaa kupewa tena projects za serikali na mkewe akawa kamchukua tayari. Remember babangu all his income zilikuwa ni project za serikali tu. All bank accounts zikawa frozen, Tanzania na Dubai......Let me end here ?
Related