Malia Obama ndani ya “hot topics”!

Ule usemi uliotumika sana na  wahenga wetu kuwa “mtoto umleavyo ndivyo ukuavyo” unaweza usilete maana sana katika kulewa watoto wa karne hii ya 21! Hivi karibuni kama wiki na siku kadhaa zilizopita binti wa Mstahafu Rais Baraka Obama, ajulikanae kama Malia Obama alikutwa akibusiana na mwanaume ambaye aliaminika kuwa ni boyfriend wake katika viwanja vya chuo kikuu cha Harvard university na pia alionekana akivuta sigara. Tazama kwenye hii video kuanzia dakika ya 22.50 kama inavyoelezewa na gwiji wa “hot topics” Wendy Williams  ?

https://youtu.be/-BwVCA4b8gw

Sipati picha Michelle Obama alikasirikaje, unaweza zimia bila “kizimio” ?? Halafu sasa kutokana na sheria za huku Malia Obama anatambulika kama mtu mzima ambaye anaweza fanya maamuzi yake binafsi na wazazi wanatakiwa kuyaheshimu! Najua hata Africa ukishafika 18+ unatambulika wewe ni mtu mzima kwenye karatasi za serikali lakini kiuhalisia wazazi wetu wengi bado wanakuwa na mamlaka juu yetu na kutufanyia maamuzi mengi juu yetu. Ni mfumo wa tamaduni zetu ambao unafanya watu wengi kutokuwa na mawazo huru na kufanya maamuzi ambayo yanampendeza yeye na kwafaida yake kwanza. Funguo za furaha zetu zipo mikononi mwa watu kama wazazi, marafiki, na jamii na ndio maana wengi ni wanafiki na waongo kupita kiasi!  Lakini vile vile lazima tukubaliane kuwa kila familia lazima iwe na identity yake! Kila mtu anazaliwa tofauti lakini kama familia lazima muwe na kitu kimoja ambacho watu watajua na kuwatambua nacho. Hivyo sishangai kwanini Michelle na Baraka wamekasirishwa na kitendo hicho. ……..Mungu atusaidie sisi ambao tunataka kuzaa na wale ambao wanalea katika karne hii ya 21 kwani changamoto ni nyingi mno!

Leave a Reply