EXTRA LIVE STRAIGHT TALK:- Nimesikia maneno mengi sana ya kujaribu kubadilisha Hoja yangu ya Msingi kuhusu kujenga nyumba ninasema tena kujenga nyumba ni jambo Muhimu sana na Bora sana ila kujenga Nyumba kama Elimu huwa sio la kila mtu kuna wanaotakiwa kulifanya lakini sio wote na inatokana na MIPANGO KWANZA .........Kwa bahati mbaya sana Wabongo tumeliweka hili la kujenga mbele sana mpaka tunaishia kushindwa kuishi Maisha yetu mpaka tunashindwa ku enjoy our lives kisa kujenga tu that I am against ...
Kama ni mfanyakazi ili ujenge nyumba unatakiwa upate mkopo na ni lazima uwe na kazi nzuri yaani umesoma vizuri so unaweza kuutumia ujira wako kwa maisha na kubakisha akiba ya kujenga smoothly sio kukosa maisha watoto wako wanateseka kisa kujenga nyumba HAPANA! ...na ndio hizo nyumba sasa hivi zinauzwa kila kona tena kwa bei poa kisa wenye majumba walikuwa wapiga dili Makazini sasa toka Magufuli awe Rais hamna madili tena mshahara hautoshi unaanza kurudi tena ulikotoka na ambako ndiko you belong kupanga kitu ambacho ulitakiwa kutumia akili mapema sana ukaenda na maisha pole pole ...
Kwa mfano mimi nilijenga nyumba nikiwa Majuu baadaye nilipokuja kupata akili ile pesa ningeweza kununua nyumba Majuu nikaiuza kwa pesa ndefu sana wakati nimeamua kurudi bongo ningeweza kujenga nyumba hata Tatu kwa pesa ile ile ambayo sasa hivi imekaa tu pale Kinyerezi for nothing ...now kuna Elimu yako na ya Watoto ambayo n muhimu sana kuliko hata Nyumba si mnawaona watoto wa wenye nyumba mlizopanga hela za kodi hazitoshi kwa mwenye nyumba kuishi vizuri na familia yake wanaishia kukimbizana na Wapangaji kuongeza kodi kila siku .... Again ninasema kila mtu na maisha yake ila mimi binafsi nitaendelea kukaa nyumba ya kupanga hapa Downtown huku nikiendelea kuwekeza na kujenga Nyumba mpya Mbweni na nitaachana na ya Kinyerezi lakini siwezi kujinyima maisha yangu kisa kujenga nyumba Mbweni HAPANA! no way ...nitapigana na maisha kupata mapato ya kutosha kuishi vizuri sasa hivi as I do and then nitaangalia kama zinatosha akiba ya kujenga pole pole lakini cha msingi ni kwanza kuishi maisha mazuri sasa hivi mambo ya kuishi kwenye lijumba halijaisha na Friji limejaa maji HAPANA! not for me! - le Mutuz Nation
Related