Kwenye maisha tunapaswa ku celebrate kila hatua ndogo tunayo piga. Kumbuka mwendo wa hatua 1000 huanza na hatua 1 so lazima ufurahie kila hatua tupigayo. Tunayo mengi ya kumshukuru Mungu hata pale ambapo bado tu matamanio mengi tu na malengo makubwa bado kutimia .Lakini lazima ufurahie hiyo safari na njiani kuna mambo madogo madogo ya kusherehekea kabla ya picha kubwa kutimia. Usiwe kipofu wa kutokuona haya madogo na ukaona hayana maana umekazana kutamani ile picha kubwa itimie ghafla kama muujiza. Utakuwa mtu wa wasiwasi, stress, kwa nini? kumbe unajitesa tu. Furahia safari yako. Furahia kila hatua.