Kwanza kabisa naomba nianze kwa kumpongeza Janet kwa mbaraka huu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu amemjalia. Hongera sana Janet Mungu azidi kuwa nawe ujifungue salama, I'm super happy for you. Najua Shiro hatokua mtoto wako wa kwanza lakini I can only imagine how happy you are kwani watoto wakike ni mibaraka mikubwa sana katika hii dunia ? Bibi yake Shiro, mama mzazi wa Janet Kisyombe Dr. Victoria Kisyombe naye alikuja kutoka Tanzania kushuhudia tukio hili, ubarikiwe sana mama yetu! Kwa kupitia account yake ya Facebook Janet Kisyombe ameandika huu ujumbe kwa rafiki yake Tumaini ambaye ndio mastermind wa hii shughuli pamoja na watu wote waliofanikisha tukio hilo ?? "BLESS ME INDEED" Peter and I are Speechless. All we can say is "THANK YOU GOD". Our Baby Shower was nothing BUT Beautiful, Stunning, absolutely Breathtaking. All this work was done by the one and only my Beautiful Sister Tumaini Kaisi-Katule (The Best Event planner/ MC /Decorator). This God Fearing Woman planned the whole event out of her Good Heart. Iska Kauga Joshua The Best photographer in East Coast, My life savior, Your work needs no Explanation. It is without a doubt done with perfection and Love. Many Thanks also Goes to KCFA Community, Love Foundation, Organizing team, and All my Beatiful sisters of TANO LADIES. Last But not Least - without forgetting each and everyone who attended our Baby shower and shower us with beautiful baby gifts. "May Our All Mighty GOD Pour Out Blessings upon each and everyone of you". #BlessMeIndeed" Baba na mama Shiro wakiwa katika pozi la picha huku wakisikiliza mapigo ya Shiro ? how beautiful! Mungu awe nanyi siku zote Kwa faida ya wasomaji wangu, najua wengi mtakuwa mnajiuliza Janet ni nani? Huyu ni rafiki yangu, ni mmoja ya watu wakwanza kabisa niliowajua hapa Marekani. Huko nyuma nilishawahi kuelezea jinsi nilivyo kutana na Janet na urafiki wetu ulipo anzia. Kama hukuwahi kusoma basi soma hapa ?? JanetKisyombe Shughuli hii ilifanyika tarehe 20 mwezi wa 10 mwaka huu huko Maryland, U.S.A Licha yakwamba Janet ni rafiki yangu, Janet pia ni Muandishi wa vitabu. Kama wewe ni mfatiliaji mzuri wa hii blog basi nahakika utakua umeshawahi kuona natoa matangazo ya kitabu kinachopendwa na wengi sana kiendacho kwa jina la "Bless me indeed"! Ni moja ya vitabu vingi vijavyo kutoka kwa Janet. Kama hujakisoma basi wahi chukua kopi yako pale Amazon nawala huto jutia!Huyu ndio Tumaini Kaisi-Katule ambaye ndio aliandaa hii shughuli yote na team yake. Yeye ndio Mc anayesifika sana, lakini kumbe siyo mtu mwenye maneno mazuri kutoka mdomoni tu, anaroho nzuri kupita kiasi. Kwa maneno yake Janet mwenyewe amenisimulia kuwa Tumaini alimwambia nakuandalia baby-shower akafikiri ni utani. Siku zilipo karibia akajua kumbe si utani ni kweli ila alijiua ni kitu kidogo tuu, kha! Kumbe hakujua anaandaliwa one of so many to come life time surprises. Janet anasema hakuchangia hats dollar moja kila kitu kimegharamiwa na dada Tumaini na baadhi ya marafiki zake Janet. Kuanzia ukumbi, mapambo, kadi za mualiko, vyakula, vinywaji n.k! Jamani, ukisema duniani hakuna waungwana mimi nitakukatalia kwani najua wapo japo ni wachache lakini wapo! Hata watakatifu wapo, kwasababu watakatifu watakao kwenda Mbinguni watatoka hapa hapa duniani! Mungu azidi kumbariki kazi za mikono ya dada Tumaini pamoja na wote waliyo shiriki katika shughuli hii wote mbarikiwe sanaaaa! Nani kama mama! Ubarikiwe sana mama yetu
Janet, asante sana kwa ku-share hizi picha pamoja nami na wasomaji wangu. Mungu azidi kukuminia baraka zake. Ukutangulie ukajifungue salama na ubarikiwe uzao wako wote ????
**Credit to**
**Wahusika wa shughuli: Peter na Janet
**Muandaaji wa shuguli nzima: Tumaini Kaisi-Katule **Mc wa shughuli: Tumaini Kaisi-katule
**Mpambaji wa shughuli: Tumaini Kaisi-katule **Photographer: Iska Kauga Joshua
Related