Zifuatazo ni picha za sherehe ndogo ambayo bibi harusi mtarajiwa Rachel alifanyia na marafiki zake wa karibu pamoja na baadhi ya ndugu zake kama siju yao ya kufurahi pamoja kabla hajala kiapo kitakatifu ambacho siyo tu kitabadilisha cheong chake to Miss to Mrs bali hata majukumu yake pia yatabadilika. Lakini yote ni kwa utukufu wa Bwana. Shere hii ilifanyika nyumbani kwa rafiki yake Rachel aitwaye Mary (kulia), huko Manvel, Texas. Rachel na Mary wamekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 20, tangu wakiwa Secondary Jangwani, wakanda wote college, wakaishi wote Wichita, Kansas, na mpaka leo hii wako hapa wote katika state ya Texas. Hivyo kutokana na urafiki wao huo ambao umedumu zaidi ya miaka 20, nanupendo wao ukiwa imara kabisa bibi harusi ameona ni vyema akawa ndio msimamizi wake mkuu katika harusi yake (Maid of honor) Picha ni nzuri na nyingi sana, hivyo nawaleta bila kuwa kwenye mpangilio maalumu. Bado
https://youtu.be/O5-LlA9BnUA
Hapo ? Rachel akitambulisha wageni na wenyeji wake. Bibi harusi aliona anajukumu la kutoa utamvulisho kwani watu wote waliofika hapo wamegusa maisha yake kwa njia moja ama nyingine. mmmh! Mahanjumati! Wadada walipika (nimesema walipika eeh ??) vikapikika haswa watu tukala mpaka vikasaza! Hii ni sehemu ya kwanza picha zipo nyingi nitawaletea zingine baadaye ??