Mgomo wa Madereva na Makondakta

1

Tumeshuhudia kwa siku mbili mfululizo mgomo ulio fanyanywa inchi zima na madereva pamoja na makondakta; kwa kweli inasikitisha sana. Embu tafakari kama kulikuwa na mgonjwa ambaye pesa zake hazimruhusu kuchukua Taxi  hivi si mtu anakufa hivi hivi?

Mimi naamini tabia ya kuto kuheshimu ajira zisizo rasmi ndiyo kunaleta haya matatizo yote. Serikali na Watanzania kwa ujumla wameshindwa kuheshimu na kutambua kua ajira zisizo rasmi nazo ni muhimu kama ilivyo kazi zingine zozote zile ambazo zinahitaji elimu ya juu. Hivyo basi kuwa na mikataba ya kazi wakati wa kuajiriwa ni muhimu kama ilivyo kuwa kwa Medical Doctor  (MD) au kwa Marketing Manager.

Hakuna kazi ambayo haina maana hapa duniani, hata kama hiyo kazi haiitaji elimu kubwa lakini inaumuhimu na inapaswa kuheshimiwa. Utakuta mtu anamdharau mfagizi wa bara bara. Hivi assume wafagizi wa bara bara pale Dar es salaam  wagome kwa siku mbili tuu; unafikiri hali ya Dar itakuwaje? Kama kwa sasa pamoja na jitihada zao lakini jiji bado ni chafu, watu wanatupa taka ovyo bila kujali machafuko ya hali ya hewa na magonjwa ya mlipuko?! Sasa wakigoma kwa siku mbili nafikiri kipindu pindu kitawamaliza wote kwa siku moja tuu!!

IMG_3480

Kitendo cha kuto kutambulika na kuwa na mikata rasmi ya madereva pamoja na makondakta ni AIBU kubwa sana kwa serikali ya Tanzania haswa katika hii karne ya 21. Kuto kuwa na mikataba ya kazi naamini kwa upande mwingine kuna changia sana madereva kuto kujali kazi zao na kupungukiwa na utu ambao zinafanya wasababishe ajali zisizo isha kila leo. Kama wangekuwa wanapewa mafunzo maalum kutoka serikalini kabla ya kuajiriwa, kuwa certified na serikali, na then kupewa mkataba rasmi ya kazi na waajiri wao basi mimi naamini hawa madereva wangekuwa makini huko bara barani na ajali zingepungua kwani mkataba wa kazi yake unamlinda yeye kama dereva (maslahi), na pia unalinda usalama wa abiria waliopo ndani ya hayo mabasi kudhurika na ajali zisizo na lazima kutoka kwa madereva wazembe.

Inchi za wenzetu zilizo endelea hakuna kazi isiyo dhaminiwa, na ndiyo maana kuna mikataba ya kazi katika sector zote za ajira. Na hakuna kazi ambayo utaipata bila kuwa na some sort of training and be certified. Hata kazi ya kulea watoto lazima kuna kozi utafanya na CPR course ni must!! Lakini embu angalia Tanzania, hivi ni waajiri wangapi huwa wanahakikisha kuwa ma housegirl wao wanajua na wapo certified kutoa huduma ya kwanza kwa watoto haswa CPR?? Je, housegirl wako yupo teyari kuokoa maisha ya mtoto wako kama akipaliwa (choked) na kitu au chakula? Je, anajua ni nini cha kufanya kama moto ukatokea ndani ya nyumba? Ukitafakari haya yote utaona sababu ya kuwa na well trained babysitter na kuweka mkataba wa kazi unaoeleweka ili kukidhi mahitaji ya kila mmoja.

IMG_3363

Nafikiri huu mgomo uwe fundisho si tuu kwa serikali kuanza kutambua na kuheshimu ajira zisizo rasmi bali hata kwa Watanzania wote kwa ujumla ambao wanatabia ya kudharau kazi za watu haswa ambazo hazihitaji elimu ya juu. Wewe msomi hunamuhitaji mzibua vyoo ili maisha yako yaendelee, wewe muuza duka unamuhitaji mbeba mabox ili maisha yako yaendelee, wewe Dr unamuhitaji muhudumu wa wodini ili maisha yako yaendelee etc….. Viumbe vyote vilivyo na uhai vinaishi kwa kutegemeana ili kuweza ku survive, tuache dharau zisizo na mpango!!

Leave a Reply