MH. LOWASSA ANAIJUA SIASA YA TANZANIA-Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a Next Speaker a.k.a Baba Pilato

Siasa za Tanzania bado hazieleweki kwa wananchi wengi na mimi nikiwemo. Wengine wanaiita siasa maji taka, siasa za kujipendekeza, siasa za mafigisu, siasa za mamluki na usaliti, siasa za propaganda, siasa za nguvu ya umma na nguvu ya dola, siasa za uongo, siasa za kidiplomasia, siasa za matukio, siasa za maigizo, siasa za maonyesho na mimi kwa sasa naziita siasa za Mwendo Kasi.Kwa Tanzania, ni Mh. Lowasa Edward pekee anaye jua siasa za nchi, anayeweza kubadili njano kuwa nyekundu, anayeweza kupanga na kupangua, anayeweza kubadilika kutokana na mazingira, anayeweza kumpenda adui yake hata kwa unafiki, anayeweza kubadili msimamo wa mpinzani wake, anayeweza kumbadili mpinzani kuwa mfuasi wake, anayeweza kupiga ngoma kisha serikali ikacheza, anayeweza kuwa na chama ndani ya chama, anayeweza kusababisha mafuriko ama hata kuyatengeneza, anayeweza kusababisha taharuki mtaani anapo onekana nahata kuwapa hofu watawala.

Kumekuwepo na kauli nyingi za kukubali ama kukataa uwepo wa njaa na uhaba wa chakula kwa muda wa zaidi ya wiki bila kuwepo kwa solution. Lakini Mh. Lowassa alipokuja na kauli ya kuwa na nia ya kutafuta chakula kwa ajili ya wahanga kwa madai kuwa Mkuu kakataa kutoa chakula kwa wahanga ikiwa ni sehemu ya kuleta suluisho la tatizo, jana serikali ikajibu mapigo kwa kusema ita sambaza chakula na ina hifadhi tosha ya chakula.

Viongozi kama akina Mh. Lowassa ni muhimu sana kwa jamii yetu hata kama wasipo weza kutawala nchi lakini uwepo wao na uwezo wao katika siasa za nchi intosha kufanya mabadiliko nje ya ya mfumo rasmi na kuleta matokeo chanya ya maendeleo..

Tutafakari kwa matendo bila hisia za vyama.

Leave a Reply