Namtukuza Mungu kwakunipa Maria, umefanyika baraka na furaha ktk kila nyakati nilizopitia,hadi kufikisha leo miaka 6 ya Ndoa.hujawahi hata siku moja kukata tamaa pale ambapo Dunia ilikata tamaa, hujawahi kusahau upendo wangu hata pale ulipokuwa mbali na familia yako. Umekuwa mnyenyekevu, mpole na mpenda Amani. Mwisho wa yote umenivumilia Kwa nyakati zote huku ukiniombea Kwa machozi na kufunga ili Mungu aendelee kuonekana katika majukumu yangu. Hakika sinachakukulipa zaidi ya kusema asante Kwa Mungu kwakunipa wewe katika maisha yangu. Bado ahadi yangu niliyoitoa tareh 23/10/2011 bado iko palepale. Endelea kuniombea na kunielekeza pale ninapokosea kwani mimi ndiye mwanao wa kwanza hapa duniani.
***Soma ujumbe wa Mr Paul Makonda kwenye 5th anniversary yao hapa ?? (MrAndMrsMakonda)***
Related