Mh. ShyRose Bhanji akiwa ndani ya Bunge la EALA. Napenda sana kumuangalia huyu dada yangu kwani ni mwanamke shujaa sana. Nimekuwa nikimfatilia safari yake katika maswala ya siasa kwa muda mrefu sana. Kwakweli nimejifunza mengi sana toka kwake kama mwanamke. Hakati tamaa, na haogopi kujaribu. Nimfano mzuri sana kwa watu haswa wanawake ambao wanafikiria kupata “shot cut” kwa kuigawa “miili” yao kwaajili ya kufanikisha malengo yao. Well, mtu anaweza sema wapo wanawake waliofanikiwa kwa kuigawa miili yao! Sasa ngoja nikwambie hao wanawake ni kama jipu linalovuja usaa halafu wao wakalipangusa kwa nje na kufunga vizuri na bandage bila kutoa “kiini” cha jipu! HAKUNA MAFANIKIO bali ni wamejiweka au kujijengea daraja la utumwa kwa wanaume! Yani siku zote hawatokuwa na amani wala furaha moyoni mwamgu kwani wanajua wako “powerless” hawawezi simama wenyewe bila kutoa miili yao. Na huwa hawafiki mbAli kabisa. Hii ni hata kwa wale wanao pata maendeleo kwa kutumia njia isiyo halali, huwa hawana amani, wala furaha, hata kama anapesa kiasi gani. Hivyo ni bora uangaike kwa jasho lako hata kama ni kwa tabu lakini matunda yake ni matamu sana. Hongera sana dada yangu Mh. ShyRose Bhanji kwa kuwa mfano mzuri kwa jamii yetu. Ubarikiwe sana. (Pichani ni Mh. ShyRose Bhanji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dr. Susan Kolimba, na mwingine ni Mbunge wa EALA).