Nuya Hellen Dausen ( @nuyahellen ) mmoja kati ya Watanzania wawili waliotajwa na jarida la #FORBES kuwa mjasiriamali mwenye umri chini ya miaka 30 (Forbes 30 Under 30) leo amezungumza katika #Clouds360 ya #CloudsTv. Akizungumzia hatua alizopitia Nuya amesema ailianza biashara baada ya Kutoka Marekani kupata mafunzo ya Uigizaji na kujikuta hana kazi kwa miezi 8 na ndipo akaanza Biashara ya vipodozi vya asili.
Nuya ambaye amesoma Masuala ya Filamu na International Trade anasema “Nilianza ‘kugoogle’ na kuangalia video YouTube ili nijifunze kutengeneza vipodozi. Nilianza kutengeneza lakini nikawa nakosea. Baadae nilipata Mwalimu huko Malaysia. NIlikwenda Malaysia ambapo nilikuwa sijui mtu huko lakini nilikutana na mwalimu wangu ambae alinifundisha vizuri nikarudi nyumbani kuendelea na biashara yangu”.
Nuya anasisitiza kuwa “Mimi nilianza kuangalia biashara hii kwa nchi za wenzetu, wao wameanza Biashara hii miaka mingi na “they are making a lot of money” Mimi niliona #Fursa huko nikaishika. Kwa Forbes kunichagua kwenye list yao, wamenihakikishia kwamba kweli ninaweza kufanikiwa”.
#Forbes wamemtabiria Nuya Hellen Dausen kwamba ndani ya Miaka 20 ataweza kutengeneza takribani Dola Milioni 200. Yeye mwenyewe anasema ataweza kupata pesa hiyo kabla ya miaka hiyo.(Sababu yeye ni #Kipepeo Anajitambua, Hana wasiwasi na Safari yake pia Anajisimamia)
Source and Credits to Clouds Media
Nuya Hellen Dausen ni msichana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 29 ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa vijana 30 wa Afrika ambao ni mabilionea wa siku chache zijazo.