Sijui ni wahenga walisema au ni waswahili walisema kuwa “mtoto uleavyo ndivyo akuavyo”, yani kuwa malezi unayo mpa mtoto akiwa ndogo basi ndiyo yatajenga tabia yake ya ukubwani. Kwa wale wanao soma Biblia basi watakuwa wanafahamu hili fungu lisemalo ‘mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapo kuwa mzee’ (Methali 22:6)
Hii amahanishi kuwa watoto wanaolelewa katika maadili mema kuwa hawatofanya makosa katika maisha yao, la hasha! Watoto siku zote watakuwa watoto na watoto wote wanapitia njia moja ya ukuwaji hivyo makosa lazima yatatokea tuu haya hepukiki.
Tofauti kati ya watoto walio lelewa katika maadili mema na wengine ni kwamba siku zote hata wakifanya makosa huwa ni rahisi kurejea katika mstari ulio sahii bila kupotea kabisa. Yani wanakua kama Kondoo aliye potea lazima ipo siku atapata njia na kurudi kundini. Kwasababu yale mafunzo na malezi uliyompa yatakua ya ‘flash’ kwenye ubongo wake kila wakati kuwa hivi sivyo nililivyo lelewa au kwa lugha za wanywe wanasemaga “I wasn’t raised this way” or “I was raised better than this” hivyo kujikuta kubadili tabia zao na kufuata mafunzo walio pewa!
Hivyo napenda kumpongeza rafiki, schoolmate, na mwanamke mwenzangu Prisca kwa malezi anayo mlea mtoto wake ya kupenda watu wote bila kujali tofauti za rangi ya ngozi zetu au maumbile yetu. Haya ni malezi mema sana na mfano wa kuigwa. Mbarikiwe sana!