Designer wa kimataifa Linda Bezuidenhout akiwa amependeza sana kwenye tukio la ufunguzi rasmi wa uuzwaji wa kitabu cha “Blended But Not Broken” cha mwanadada maharufu sana jijini Atlanta, Georgia ajulikanaye kama Sasha the Diva! Ambaye pia ni mtangazaji wa radio (Kiss 104 FM) maarufu sana hapo hapo Atlanta……. kama kawaida yake Linda alikuwa amevalia mavazi mazuri ya LB designs ambayo amebuni na kushona yeye mwenyewe. Nywele zake na makeup alipambwa na celebrity stylist MUA @stylesby_crave ….. alipendeza sana Linda pamoja na mumewe Mr Mali Kimesera walikuwa moja ya watu muhimu walio alikwa katika hafla hiyo ambayo ilifanyika siku ya tarehe 12, May, 2016 kwenye ukumbi wa The Ventana Room, downtown, Atlanta, Georgia. … pichani ni muhusika mkuu wa siku hiyo Sasha the Diva (ambaye pia ni mteja mkuu wa LB) pamoja na Mr and Mrs Mali Kimesera. Hapa Mr and Mrs Mali Kimesera wakiwa na Mayor wa jiji la Atlanta bwana Kasim Reed wakati wa ufunguzi wa kitabu hicho “Blended But Not Broken” cha Sasha the Diva of Kiss 104 FM. Ms LB pamoja na Mayor Mr. Kasim Reed Picha nzuri sana. Walipendeza mno!…… Picha zote na @jaxonphotogroup