New couple in town ? Kwanza nianze kwa kuwapongeza maharusi Ken and Christine kwa kuachana na maisha ya u-bachelor na kuamua kufunga ndoa takatifu siku ya JumaMosi tarehe 11 mwezi wa 08 mwaka 2018. Ndoa hii takatifu ilifungwa kwenye Chaple ya Sterling Banquet Hall lililopo Houston, Texas. Ambapo ilifuatiwa na sherehe nzuri sana kwenye ukumbi huo huo. Tunawaombea neema nyingi kwenye ndoa yao, Mungu akawe kiongozi wao siku zote, ndoa yao ikajae amani na furaha nyingi sana. Wakabarikie na uzao wa tumbo lao hata kizazi cha tatu na cha nne. AMEN Kwafaida ya wasomaji wangu, bwana harusi ni rafiki yangu wa miaka mingi tuliishi wote Kalamazoo, Michigan, huwa napenda kuwaita “my Kalamazoo family members” kwani tuliishi kwa amani na upendo. Kwasasa yeye anaishi Dallas, Texas na mimi naishi Houston, Texas. Bibi harusi yeye alikuwa akiishi Spring, Texas lakini sasa amekuwa mwana Dallas, Texas kwani huko ndiko makazi yake mapya. Gosh! Ain’t they pretty ? Wasimamizi wa kiume na bibi harusi katika pozi. Kutoka kushoto ni Sammy: yeye alikuwa ndio Bestman. Nirafiki wa bwana harusi wa miaka mingi sana toka Kalamazoo, Michigan na sasa wanaishi wote Dallas, Texas.
Anayefuata anaitwa Gittu: Yeye pia ni mmoja wa “Kalamazoo family members”. Nirafiki wa bwana harusi wa miaka mingi toka Kalamazoo na sasa wanaishi wote Dallas, Texas.
Na huyo gentleman wa mwisho anaitwa Charles Nyakure kutoka Dallas, Texas ni rafiki mwema wa bwana harusi. Naye tumemu adopte kuwa mmoja wa “Kalamazoo family members” ?? Mmenionaa ?? mimi hapa upande wa kushoto, mwanangu upande wa kulia pamoja na Mr and Mrs Sande Dada wa bwana harusi all the way from Nairobi, Kenya akiwa na bestman-Sammy Wazazi! Kutoka kushoto ni baba mzazi wa bibi harusi. Anayefuata ni dada wa bwana harusi. Mwenye nguo ya blue ni mama mzazi wa bibi harusi, na wa mwisho ni baba mzazi wa bwana harusi. Wote wamekuja rasmi kutoka Nairobi, Kenya kwaajili ya kushuhudia tukio hili takatifu. Picha zote kwa hisani ya Charles ?…… Thank you so much Charles be blessed!