“Nakumbuka kama miaka sita nyuma nilikuwa msichana tu, tena msichana nisie na ndoto hata za kuwa na mtoto, msichana niliyekuwa na picha tofauti juu ya wale wanaozaa, msichana nilieona kila aliezaa amepoteza Dira, kiufupi ni kama shughuli imeisha.
Lakini leo nimezikana hisia zangu mwenyewe baada ya kuwa na watoto (sio hata mtoto mmoja) ninapogundua kumbe maisha ndio YAMEANZA, kumbe kuna raha ambayo hata ningehadithiwa bado nisingeweza kuelewa hisia zake, kumbe hakuna kuchoka, na zaidi lwa wale walio single Mamaz bado una nafasi ya kutakwa na yoyote yule na akakuona kama bado wa jana na kukuheshimu na kukupa thamani ya hali ya juu, kiufupi unaweza hata ukawakimbiza ambao hawaijui leba ?? na yote ni kwakuwa bado unapendeza, bado unavutia, hakuna kilichopungua zaidi ya kuongezeka kiufupi ni hisia tamu mno
Kama wewe ni MAMA na unajivunia kuwa MAMA huku ukiendelea bado kujiamini embu nyoosha mkono juu!! Nafikiria kuandaa kitu cha kutukutanisha WAMAMA WOTE WA KISASA ambao hawajajitupa na huku bado wako proud na UMAMA wao iwe siku ya kuonyrsha how fabulous you are hata kama una mtoto / watoto, iwe ni siku yetu ya kujidai na kupendeza, iwe ni siku ya kuprove wanaona kuzaa ndio kuisha na kuchoka…Bila kusahau RED CARPET MOJA YA HATARI MNOOOO.
WANGAPI WANGEPENDA KUSHIRIKI KITU CHA NAMNA HII!!?? SEXY MAMAS ARE YOU OUT THERE!!??” Zamaradi Mketema
MAONI YANGU MIMI ALPHA: Sijashangazwa na mtazamo ambao Zamaradi alikua nayo huko nyuma. Kwani hivyo ndivyo govt. System nyingi za Africa zimeweka mfumo wa kuwafanya wasichana walio zaa bila ndoa kuwa hawana maana wala faida kwa jamii. Na hii mifumo ya serikali zetu inaundwa na jamii zetu husika ambazo ni jamii zilizo jaa fikra potovu za kuhukumu na kuadhibu watu bila kutafuta chanzo na suluhisho la tatizo liliopo. Kuzaa sio mwisho wa maisha! …….Enjoy the party!