Kamanilivyosema kwenye posti yangu iliyopita somahapa yakwamba mwaka 2022 ulikuwa na baraka zake nyingi sana. Basi katika kuhesabu mibaraka yangu naweza sema huu nao ni moja ya mbaraka mkuu. Ni jambo ambalo lilinifurahisha zaidi ππ Ni surprise niliyo wafanyia wazazi wangu.
Tarehe 25 mwenzi wa Saba, mwaka huu wa 2022 (07/25th/2022) ilikuwa siku ya furaha sana baada ya mipango yangu ya kuwafanyia wazazi wangu haswa mama yangu safari ya kuwasalimia bila ya kuwapa taharifa kama ilivyokua huko nyuma. Nimpango ambao nilipanga na mdogo wangu aitwaye Magreth Otieno Igogo a.k.a Mrs Jacob Massawe kuwa tutamfanyia mama surprise wakati wa siku yake ya kuzaliwa ambayo ni tarehe 27th July. Bahati mbaya ratiba yangu ilibidi nifike siku mbili kabla ya birthday yake. Mimi nilichukua likizo na kuandaa safari bila kumwambia mtu yoyote nyumbani isipokuwa mdogo wangu, mume wake na mwanangu tu. Sikutaka mama ajue kabisa hivyo kuzuia wanafamilia wengine kujua hata marafiki ilikuwa muhimu sana. Nashukuru Mungu kila kitu kilikwenda vizuri kama tulivyopanga tuliomba kibali cha Mungu kwa kumkabidhi mipango yetu naye akaibariki ikatimia. πππΏπSafari yangu ilianzia Houston, Texas.
Nakumbuka siku nakwenda airport tulimpigia mama simu, akiwa nyumbani na baba na shangazi yetu fulani wakipiga story zao, nikaanza kumuuliza anampango gani na birthday yake?! Akawa anasema nahamu namtoko fulani amazing π π lakini ameshapanga kwenda Fun city na watoto wake wa shule (school trip). Nikamwambia kwautani nikikutumia Dola Mia ($100) uongezee kwenye hiyo trip itatosha? akasema itatosha sana. Nikamwambia basi nitakutumia tarehe 25, ambayo ndio tarehe nilikuwa najua naingia nyumbani. π π π Basi nikamalizia kwa kumwambia wakifunga shule apange trip yeye na wadogo zake na dada zake waende kutembea Zanzibar au mbuga za wanyama, wafanye bageti halafu anijulishe. Akashukuru kweli kweli bila kujua mimi hapo naingia uwanja wa ndege teyari kwa kum-surprise! ππ
Sasa, ilikuhakikisha chumba changu kipo katika hali nzuri mdogo wangu alimdanganya mama kuwa ana wifi yake anakuja toka Japan na ana mtoto mdogo hivyo anaomba aandae chumba cha dada Alpha (eeh usishangae sana, nina chumba changu kwa mama yangu ππ) ili afikie humo kwa siku kadhaa kabla ya kwenda Moshi. π π mdogo wangu wanaishi nyuma tu na kwa mama. Basi mama naye bila shaka wala kinyongo akamkubalia pasi kujua mwenye chumba yupo njiani. π π Nilipofika airport nilipokelewa na mdogo wangu pamoja na mume wake. Tukiwa njiani mdogo wangu akampigia mama simu akamdanganya kuwa amekutana na rafiki yake walikuwa wote huko kijijini Kowak (kijiji alipozaliwa mama yetu), na anasema hawezi kwenda kwake mpaka afike kumsalimia. Mama akanza kuuliza ninani? mdogo wangu alikataa kata kata kusema akamwambia ni surprise akifika hapo itabidi asikilize sauti yake ili amtambue ni nani! Mama alimbembeleza sana amwambie ni nani huyo lakini mdogo wangu alishikilia msimamo kuwa utamuona wakifika. Mama kidogo akawa kama amechukia kwani alikua anasema unakuja na mgeni mimi hata kupika sijapika hata juice ndo kwanza wanatengeneza sio vizuri na hapendi kabisa. π π mdogo wangu hakubadilisha msimamo wake mpaka tukafika nyumbani, na mengine yote yamebaki kuwa historia kama hiyo video ya tukio hilo inavyo onyesha. π π
Hii ni mara ya pili sasa nafanikiwa kuwa-surprise wazazi wangu. Tarehe 07 mwezi wa tatu, mwaka 2017 kwa kushirikiana na wadogo zangu pamoja na baadhi wafanyakazi wa Utegi Technical Enterprises Ltd (kampuni anapofanyia kazi baba yetu) tulifanikiwa kum-surprise baba yetu ofisini kwake, ilikuwa siku ya birthday yake. ππ Tuliwahi sana ofisini kabla yake kitu ambacho hajazoea kwani siku zote yeye ndio anakuaga wakwanza kufika. Tukaingia ofisini tukazima taa sehemu ya mapokezi ili akiwa kwa nje ajue hakuna mtu. halafu tukamwambia mlizi arudishie tu mlango asifunge na funguo, na geti arudishie bila kuweka kufuli ili akifika tu ashtuke na akasirike (just to annoy him) kuwa waliacha mlango na geti wazi jana jioni. Sasa alipofika mlangoni anakuta ipo wazi akasema ooh! Tumesha ibiwa hapa, hasira zikamshika kuwa geti halikufungwa jana jioni. Halafu mdogo wetu aitwaye Guka ndio tulimuacha nje awe ana mmonita (monitoring him) kwa kutupa taharifa kwa simu kuwa ameshafika kwa parking lot. π π Na Guka alikuwa anawasiliana na dereva kusema wapo wapi. π π Tazama video hapo chini ππΏπ π
Basi, alipopita tu mapokezi kuingia eneo la secretary wote tukasema “surprise” kwa nguvu na furaha huku mmoja wetu alikuwa kwenye switch ya kwashia taa, tukaanza kuimba “happy birthday to you” π π π alishangaaje, hasira zote zikaisha hapo hapo. π π π π Hakuamini kuwa watu waliweza kuwahi kazini mapema hivyo ilitu wam-surprise! Alishukuru sana na furaha nyingi mno.
unaweza itazama video yote ya surprise kwa kupitia YouTube yangu hapo chini ππΏ
Kwakweli ni furaha kufanya jambo ambalo linamfanya mtu mwingine kuwa na furaha na kujisikia vizuri kwa kujiona mwenye thamani, lakini nifuraha zaidi kufanya jambo linalowafurahisha wazazi wako. Nafurahia na najisikia vizuri pale ninapoweza kuwafanya wazazi wangu wafurahi zaidi. Ni mbaraka wa pekee. ππ Counting my blessings ma’am! π π
Na story zitaendelea maana mama Igogo alikuwa haamini alichokiona. ππ
Surprise ya mwisho iliharibika π π tulitaka dada yetu naye am-surprise mama lakini dakika za mwisho akaamua kumwambia kua anakuja halafu hata hakutuambia kuwa kamwambia mama hivyo ikawa surprise kwetu. π π ππ kwakweli hii ni the best moment for 2022.
Miaka takriban 3 iliyopita dada yangu naye alim-surprise mama big time. Alikuwa mjamzito na wakati uchungu umeanza akampigia mama kumsalimia basi wakaagana vizuri. Ndani ya masaa 2 mume wake anampigia mama simu kuwa mama Dani amejifungua mtoto wa kike na wameamua kumrithisha jina la mama. Mama akawa hataki kuamini anasema mbona mama Dani nimeongea naye muda sio mrefu? π€£π€£π€£ akaambiwa pale anakupigia alikuwa ameshikwa na uchungu na tulikua njia kwenda hospitali. π π Na mtoto mwenyewe ndo huyo hapo ππΏ juu. π€©π€©