Habari ya mama aliyeuguliwa ghafla na mtoto wake majira ya SAA 2 usiku, mtoto alibanwa na kifua(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda kuomba msaada kwa jirani yake aliyekuwa na gari, akamjibu gari haina mafuta, akaenda kwa mchungaji ili amsaidie, akamjibu nina wachungaji toka USA, hivyo sitaweza kuwaacha peke yao, mama hakuwa na jinsi aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije kufa kama baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo. Huyo mama alikuwa na tatizo la mguu na mtoto alikuwa mzito, mama alianguka Mara kadhaa na akainuka kuendelea na safari. Njiani alikutana na watu waliotoka kazini aliomba wamsaidie walimpuuza na alijaribu kusimamisha magari hayakusimama. Kichaa mmoja mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani alipomuona yule mama anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali. Ma doctor walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura, wakamchukua mtoto na kumhudumia haraka, baada ya dk.10, mama wa mtoto akawasili, kisha ma doctor wakatoa taarifa kuwa, mtoto angecheleweshwa dk 5 angekufa. Mungu alimtumia yule kichaa mchafu kuokoa maisha ya mtoto. Hivyo usimteegemee Mch, jirani, wenye magari, matajiri nk. Mungu huweza kuinua MTU usiyemdhania kukubariki. Mwamini Mungu atakubariki. Usitumainie wanadamu hakuna baraka kwao. Mungu huinua vinyonge ili kuangusha vyenye nguvu.