Wapendwa wasomaji wangu nimekua mvivu sana siku hizi kuandika humu! Natafuta pesa wapendwa, mambo ya kuandika magazeti humu wakati bank kunasomeka negative zero hata hainogi ?? Lakini kama mjuavyo huu si ni mwezi June!! Sasa nitaachaje uwanze bila kuandika kitu humu. Huu sindio mwezi tuliozaliwa viumbe wenye roho za kipekee, viumbe wenye upendo mwingi kuliko viumbe vyote duniani! Viumbe tusiojua kuangaika na mambo ya watu, viumbe wenye furaha na amani muda wote. Viumbe wenye akili za ziada na utashi (Intelligence) wa hali ya juu! Viumbe vinavyo penda kujitegemea zaidi, viumbe vinavyo chukia majungu na umbea ?? Viumbe vinavyo jali na kuheshimu hisia za watu. The Legends ??? Yani ni viumbe fulani amazing kinoma and I am proud of myself to be one of them!
Unaona hiyo picha hapo juu baba mzazi kashanipa baraka zake za kuanzia mwezi. Basi nami naomba niwatakie kheri na baraka zote za mwezi huu wa Sita. Wale tulio zaliwa ndani ya mwezi huu nawatakieni birthday njema, Mungu akawabariki sana ukawe mwaka wa kheri nyingi sana katika miezi iliyo bakia. Mbarikiwe wote. June born babies we truly Rock! ?❤❤