Harriet Shangarai ni Mtanzania aishie Maryland, U.S.A Yeye ni Registered Nurse (RN) mwenye Bachelor degree of science in nursing (BSN). Harriet pia ni mmiliki wa blog ya nesiwangu.com, ambapo katika blog hiyo anaongelea na kufafanua magonjwa mbali mbali kwa njia ya lugha ya Kiswahili kwani yeye anaamini information is powerful (yani kuwa na ufahamu juu ya jambo linakufenya au linakupa ujasiri) hivyo anajaribu kuwapa Watanzania hujasiri wakujua miili yetu na kuwa na ufahamu wa mabadiliko ya miili yetu mara tuu utakapoona kitu chochote au hali yoyote ambao si yakawaida hivyo inakupa nafasi ya kuchukua hatua muhimu kama kumuona doctor.
Harriet si tuu anafafanua kuhusu magonjwa na dalili zake, bali pia anasaidia watu kujua wapi unaweza kwenda kupata msaada au huduma unayo hitaji haswa kwa Watanzania waishio Maryland. Yeye pia ni Makamu wa Rais wa jumuiya ya District of Columbia, Maryland , na Virginia (DMV), anatumia sana elimu na experience aliyo nayo kuweza kusaidia wana diaspora wenzake ambao wanahitaji msaada wa kijamii. Kwa mfano, (bonyeza link hapo chini) unaona jinsi alivyo fafanua ugonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi, dalili zake na hatua za kuchukua.
http://www.nesiwangu.com/saratani-ya-shingo-ya-kizazi/
Jamani, hivi ushawahi kukutana na mtu kwa mara ya kwanza halafu ukahisi kama ndugu yako au rafiki uliyemfahamu kwa muda mrefu?! Basi hivyo ndivyo nilivyo jisikia siku ambayo nilikutana na Harriet. Ni mwanamke shujaa na mnyenyekevu wa hali ya juu, mwenye ukarimu usio elezeka. Yani kwakweli huyu dada ANA MOYO WA MALAIKA! Ubarikiwe sanaaaaa Harriet, najua tabia yako na moyo ulionao si wakuiga bali ndio hualisia wako na naamini hivyo ndivyo utakuwa mpaka siku Mungu akikuita. Naamini watu wengi wataponjwa kwa kupitia wewe, Mungu ameamua kukutumia wewe kuonyesha upendo na ukarimu wake ambao dunia kwa sasa unahuitaji kuliko ilivyo kuwa zamani!
Hivi karibuni mtakuja kumsikia Harriet kwa mdomo wake mwenye akiongelea maisha yake, changamoto, na mambo mengi aliyopitia na kufanya mwanamke, mama, na mke aliye sasa. Ninini kilimfanya akaamua kuingia katika field ya afya na mambo mengine mengi yahusiyo jamii.
Basi kwa kujifunza zaidi kuhusu afya yako tembele blog yake ya www.nesiwangu.com