Watu huwa wanasema kuwa ukitaka kujua tabia halisi ya mtu subiri akipata pesa au akipata nafasi ya kuwa kwenye position ambayo inampa power (madaraka ya juu). Kuna baadhi ya watu wakiwa na maisha ya kawaida au nafasi za chini kwa sababu fulani huwa wanapenda sana ku pretend na kuonyesha tabia ambazo si halisi najinsi waliyo. Matendo yao huwa nitofauti na matamanio ya myoyo yao. Utakuta mtu anakuwa mcha Mungu sana na mtu mwenye maadili ya hali ya juu na watu wengi wanamuona kama malaika, lakini mtu huyo huyo akipata hela au madaraka kidogo huwa anatoa makucha yake au kuonyesha tabia yake halisi na watu wengi huwa wanaishia kushangaa kwasababu huwa ni tofauti kabisa na walivyo mzowea.
Kama umeweza kupata nafasi ya kusililiza mahojiani aliyofanya Sporah na Emelda Mwananga katika Sporah Show, basi utakua umesikia kuwa “Jacqueline Mengi” amemfungulia mashtaka Bang magazine kwa kile kinacho onekana kama wamekwenda kinyume na matarajio yake. Kwa maelezo ya Mkurugenzi wa Bang Ms. Emelda Mwamanga ameeleza kuwa alikuwa anafahamiana na Jacqueline kabla hata ya kuolewa na Dr. Mengi, vile vile alishawahi wahi kumfanyia mahojiano huko nyuma ambapo aliongea mambo mengi yanayo husu maisha yake binafsi kama engagement (nafikiri hapa ni ile engagement yake na mtoto wa Kingunge Ngombalemwilu) na mahusiano aliyokuwa nayo na wanaume wengine kabla ya kuolewa na Dr. Mengi; hivyo hili swala la kupelekana mahakamani limemshangaza sana kwani nikitu ambacho wangeweza kuzungumza na kuyamaliza.
https://youtu.be/b32iJhfcX2w
Kiukweli hata mie nakubali kuna makosa ambayo yametendeka lakini swali ambalo najiuliza je kweli yalikuwa ni makosa ya kufikishana mahakamani, especially kwa watu walio kuwa wanafahamiana? Au ni kiburi cha pesa? Je the so called “Mrs. Mengi” ni mkarimu na nyenyekevu kama Watu wengi huko nyuma walivyo kuwa wakimsifia kuwa Jacqueline ni mtu mzuri sana, hana maringo. Sasa sijui kama kuwa “wife” wa Mr. Mengi kumembadilisha tabia au ni mtu aliyekuwa amejificha makucha yake na sasa anaona ni wakati muafaka wa kutoka out of the closet kwasababu ni “mke wa bilionea”. Mimi sijui sina huwakika, labda nawe angalia hiyo show and be the judge! Japo kwasasa Watanzania watapata nafasi ya kumjua Jacqueline halisi 🙂 because you can’t pretend forever!
Kitu ambacho naona MD wa Bang magazine ameongea kwenye public na hakupaswa kusema ni kuhusu policy yao ya kuto kuonyesha nakala au kutuma picha kwa watu walio fanya nao interview baada ya naakala kuandikwa. Ila inaelekea hiyo policy inakuwa waived kwa baadhi ya watu walio wafanyia interview kwa sababu wanawaheshimu “kwaheshma unajua si kwa wote sisi unajua tuna policy kwamba ukisha fanya makala sorry umemfanyi interview mtu haupaswi kutuma tena picha au maswali ni very rare na kwa watu ambao tunawaheshimu sana anapo request ile interview imeshaiandika naomba niipitie tuanampatia …..” Kwakweli hii haikupaswa kusemwa in public kabisa haswa ukizingatia ni kinyume cha poilicy zenu. Hii itafanya watu walio fanya interview na nyie na hawakupata kupewa hiyo nafasi wajione kama hawakuheshimiwa na hawakuwa na umuhimu kwenu. Na hata huko mbeleni kama hamkuwapa watu hii chance wakati wamesikia ukisema kuwa kuna baadhi ya watu huwa mnawapa hiyo special treatment kwakweli sidhani kama watafurahiya hata kama ni wachache ndo wanapewa swali litabaki kwa nini wao na si mimi? Hili hukutakiwa kusema, ulikosea sana.
Mahojiano yalikuwa mazuri sana, nimependa sana alivyo ongelea kuhusu maadili ya Mtanzania na kuwasihii wasanii wazingatie hayo. Inafurahisha na kuvutia kuona dada mzuri na kijana kama Emelda anajitambua na kujua nafasi yake katika jamii. Hongera sana Emelda!