Nimekuwa nikikosa usingizi kwa wiki nzima tangu Pilato aje duniani na hii inatokana na huduma ya mama na baba kwa mtoto mchanga mda wote hasa usiku maana pilato bado hajajua majira ya duniani yakoje. Lakini leo majira ya saa tisa usiku nilikamatwa na usingizi mzito ulionichukua na kuniburudisha na ndoto ya matumaini kwa watu wenye ulemavu. Hii ni ndoto ya pili inayotaka kufanana ila hii ya sasa imejumuisha kundi kubwa la watu wenye ulemavu. Kwa waafrika ndoto zina maana sana na hasa kwa kabila letu la kimataifa la LUO. Hata maandiko na adithi za mitume inaonesha jinsi ndoto ilivyotumika kutoa taarifa kutoka kwa Mungu kwenda kwa mitume wake.
NDOTO yenyewe iko hivi…
“Nimejikuta nipo shule ya Pugu Secondary nikiwa kama mwanafunzi, (kwa historia fupi hii ndio shule yenye mazingira na baadhi ya miundombinu inayo support wanafunzi wenye ulemavu wa kiume jijini Dar, na ndio shule ambayo nimepata elimu yangu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita mchepuo wa Sayansi PCB). Ndoto inaonesha Mh. Raisi JPM anatembelea shule hiyo gafla tena alfajiri ya saa 12 tukiwa tunaamka. Pugu sekondary ina mabweni mawili ambayo ni maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu, hivyo ndoto inaonesha Mh.JPM alifikia moja kwa moja katika mabweni yetu na wanafunzi wote tuliokuwemo tukapatwa na mshangao huku tukiwa na furaha sana ya kutembelewa na Mh.JPM. Kama kawaida ya JPM alianza na maswali yake ya kutaka kujua hali halisi ya Elimu tuayopata hapo shule, tulimueleza mengi yaliyogusa changamoto za mifumo ya elimu kwa watu wenye ulemavu na tukatoa na mapendekezo ya jinsi ya kupunguza changamoto hizo kama sio kuzimaliza kabisa. Mh.JPM alikuwa msikivu na alionesha sura ya kuguswa sana na maelezo yetu watu wenye ulemavu juu ya umuhimu wa Elimu kwa watu wenye ulemavu.
Baada ya hapo Mh.JPM alinigeukia na kutaka mazungumzo na mimi, (Oooh May God) nilishituka nikupatwa na wasiwasi na fikra ya kutumbuliwa lakini nikajipa moyo na kujikaza kisabuni kisha nikasema moyoni (sina makosa ngoja nimsikilize).Mh. JPM alianza kwa kunipongeza juu ya makala zangu ninazozitoa katika mitandao ya kijamii akisema kuwa na yeye huwa anazisoma na kuzifurahia. Baada ya pongezi Mh.JPM akanipa jukumu moja la kuandika makala za kueleza changamoto za watu wenye ulemavu Tanzania, Mh.JPM akaenda mbee zaidi kwa kusema niwashirikishe waandishi wengine kama Yericko Nyerere, Magoiga SN, Binti Tanzania, na Malisa katika kuibua changamoto zinazowapata watu wenye ulemavu bila kujali itikadi maana Mh.JPM alisema hata wao wanaguswa na kundi hili. Baada ya agizo hilo Mh. JPM na wasaidizi wake walituaga na kurudi kwenye magari yao tayari kwa safari ya kwenda Ikulu, gafla nikapata wazo la kupiga picha na Mh. JPM lakini nikiwa najiandaa kuvaa nguo nzuri kwa ajili ya picha nikasiki muungurumo wa magari yake meusi kuashiria Mh.JPM alikuwa anondoka. Moyoni niliumia sana kukosa kupiga picha na JPM na ndio maana nikaona niweke picha ya ndoto yangu ya kwanza iliyofanikiwa kutimia na kupiga picha. Baada ya hapo nilishitushwa na kelele za mwanagu Pilato akiwa analia kuashiria tatizo. Tafsiri ya Ndoto…(kwa maoni yangu
1. Ndoto imebeba ujumbe na taarifa mahususi kwa watu wenye ulemavu juu ya utayari wa JPM katika kutatua matatizo ya walemavu. Inabidi tuamke na kueleza.
2. Ndoto inakumbusha jamii kushiriki katika kupaza sauti za watu wenye ulemavu bila kujali itikadi ili kuibua matatizo yanatukumba watu wenye ulemavu
3. Ndoto pia inaonesha kuwepo kwa ziara ya gafla ya JPM kwa shule zenye mazingira na miundombinu inayokidhi watu wenye ulemavu. (Hivyo walimu wakuu wajiandae ???)
#Mytake.
Jamii ya watu wenye ulemavu inakuwa kwa haraka kutoka na majanga ya ajali na magonjwa, na nina hakika kila mtu anaguswa na jamii hii maana tumefika 4M, hivyo natoa wito kwa jamii kupaza sauti kwa ku comment na ku share ili imfikie Mh.JPM na serikali aliyoiunda na kumpa taarifa kuwa watu wenye ulemavu tuna imani na yeye na tumeona nia yake ya kutuinua juu.
Asanteni sana
#TanzaniaDisabilityEmpire, #JukwaaLaWalemavuTanzania
#ElimuKwaWalemavu