Imezoeleka katika bunge letu tukufu kusikia kelele za lawama na za kukosoa mipango na utendaji wa serikali kutoka kwa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani. Kelele hizo zimewahi kusikika na kuibua kashfa nyingi na kukosoa sera, sheria, mipango na hata utendaji mbovu na hata kusababisha maamuzi magumu ya kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi na wengine kujiuzuru nadhifa zao kama ilivyokuwa kwa Mh. Edward N. Lowassa. Lakini pamoja na hayo kufanyika bado serikali ilifanikiwa kupita majaribu hayo yaliyokuwa na wakati mgumu. Serikali iliweza kufanikiwa siku zote kupitia umoja na wingi wa viti vya wabunge walivyokuwa navyo bungeni maana waliweza kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Hoja nyingi za wapinzani zilifunikwa kwa kura nyingi zilizokuwa zina maslahi ya kificha aibu ya chama na serikali.
Katika Bunge la kipindi hichi, mambo yamekuwa tofauti sana hasa katika kupiga kelele. Kelele nyingi na zenye uzito zimepigwa na wabunge wa CCM na zimepata Kick kuliko hata kelele za Upinzani. Ukiangalia wabunge waliokuwa vinara wa kutetea serikali wamefika mahala wamegeuka na kupiga kelele.
Maeneno mengi ambayo yamepigiwa kelele ni kama yamewakera wengi mpaka yameshindwa kuvumilika. maeneo kama uchumi, afya, demokrasia na utawala bora. Kelele hizi zinawwza kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama tawala na serikali inaweza kupata vikwazo vigumu katika kutekeleza wajibu wake.
#Myatake
1. kuna uwezekano kuwa wabunge wanabanwa na wanachi wao na hata wao kupata wakati mgumu kuliko kipindi kingine, hivyo hasira zikawarudia serikali.
2. Yewezekana wabunge wa CCM hawasikilizwi katika mapendekezo na ushauri wanao toa kwa serikali ama serikali haitoi ushirikiano kwa wabunge wake
kuna msemo unasema kuwa adui mkubwa ni yule anayepatikana nyumbani kwako kuliko anayepatikana kwa jirani, Kuna haja ya serikali kujitathimini ili kulinda maslahi ya kutawala nchi lasivyo Jahazi litasumbuliwa na abiria wenyewe.
Asanteni sana
0713037798