**Sehemu ya Kwanza**
WAKATI NI UKUTA: Katika Dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano, WAKATI(Time) ni jambo la kuwekewa umakini mkubwa kupitia tafiti na uchunguzi wa jambo lolote lile unalotaka kulifanya. Wakati una tabia mbilimbili. Wakati haurudi nyuma wala hauna haraka, Wakati hunena na kuamua jambo, Wakati hutibu na kuzalisha vidonda, Wakati huishi na kufa, Wakati huelezea historia na kutunza, Wakati hutabiri yajayo na kutimiliza, wakati ni kipimo cha udhaifu na uimara, Wakati hutenganisha watu na kuunganisha, Wakati ni kiungo kwa mambo makubwa na madogo.
Wakati una nyakati nyingi na kila nyakati una zama zake na kila zama zina mambo yake. Leo naomba nivae viatu vya Mtu Huru kumwambia Mbowe kama Mkuu wa Chama mbadala (CHADEMA), Ni kweli kazi mliyoifanya kwa miaka zaidi ya 20 ya kujenga fikra mbadala katika siasa za Tanzania ni kubwa na yenye kuhitaji kupongezwa kwa moyo wa dhati kabisa (Hongereni sana). Lakini nasikitika kusema kuwa kazi yote hii ni kama 30% kati ya 100% ya wajibu wenu mlioamua kuutimiza juu ya siasa za nchi. Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda vitu, matendo na fikra tofauti zenye kubadili mitizamo, imani na mienendo ya jamii maana naamini kuwa “FIKRA Tofauti Huzaa UBUNIFU na Ubunifu ndiyo chanzo na chachu ya MAENDELEO katika jamii”. Nchi yetu ipo katika nchi zinazofanya siasa za kuigiza, Siasa za majukwaa, siasa za propaganda, siasa za Ukweli kugeuka Uongo na Uongo kugeuka Ukweli, Siasa yenye kibwagizo cha Demokrasia, Siasa ya matabaka ya uelewa na vimelea vya Ubaguzi, Siasa ambayo mpinzani anatumia Chuki na vugurgu kutafuta madaraka na Mtawala akitumia vyombo vya Dola kulinda Madaraka yake, Siasa ambayo vyama vyake hutegemea Umasikini na Ujinga wa wananchi kama Mtaji wao, Siasa mabazo mifumo ya nchi huegemea upande mmoja, Siasa ambazo mwanasiasa anawekeza katika chama kuliko waliomchagua, Siasa zisizo na mabadiliko ya mbinu, Siasa za kungojea Marekani na Uingereza wamefanya nini ndipo nasi tuige, Siasa zisizo zungumzia ISSUES na badala yake zinazungumzia MATUKIO, Siasa zenye kulenga kizazi kilichopo tu badala ya kwenda zaidi kwa vizazi vijavyo, Siasa zenye kunukuu Fikra za Mwl Nyerere kama kikomo cha Fikra badala ya kuja na Fikra pevu zaidi, Siasa iliyoacha kutilia mkazo masomo ya siasa na uraia kwa vijana, Siasa ya UBEPARI katika nchi ya UJAMAA yenye mifumo ya utendaji ya URIBALELI…
Mtu huru anawezaje kufanya siasa katika nchi kama hii na ategemee kupata matunda huru? Nchi ambayo wananchi (wapiga kura wake) hawana uelewa juu ya HAKI na WAJIBU wao katika nchi, Hawajui kutofautisha ukweli na propaganda, Hawajui kutofautisha ushabiki wa vyama vya michezo na siasa, Hawajui mipaka yao wala ya watawala wao, Nchi ambayo mfumo wake kwa mwananchi tangu anazaliwa mpaka anazeeka ni Mtegemezi tu, Nchi ambayo walinzi wake ni wale ambao hawakufanya vizuri shuleni na wale ambao walikuwa ni wakorofi, majasiri na watukutu shuleni.
Kuna jambo Mtu huru amelisahau ambalo ni la muhimu sana kwa nchi kuwa huru. Apo ndipo WAKATI unapobadilika na kuwa UKUTA, Wakati wa siasa za chuki kwa vyombo vya Dola umepitwa, Wakati wa kuwaandamanisha wananchi wanyonge umeshapita, Wakati wa siasa za matukio umepita, Wakati wa siasa za migomo umepita. Kama Mbowe na timu nzima ya upinzani bado wana siasa za namna hii basi wajue kuwa wamefikia UKUTA na wana haja ya kubadilika.
Ningekuwa mimi ninkiongozi wa Upinzani kama alivyo Mtu Huru MBOWE basi ningefanya yafuatayo….
1. Ningewekeza na kuanzisha operation kwa wananchi za kutoa ukungu wa kuelewa haki na wajibu, siasa na uraia na kuwapa uelewa zaidi wa kijamii ili wawe huru na waweze kuja na fikra huru na mbadala katika nchi. Kwa sasa bado watanzania wengi hawajui mambo mengi ya siasa na hivyo maamuzi yao mengi yamekuwa ni ya kuiga na kufuata mkumbo.
2. Ningewekeza katika kurudisha mahusiano ya karibu sana na vyombo vya ulinzi na usalama. MBOWE, Huu sio Wakati wa kushindana na vyombo vya usalama ambavyo hata wao wengi hawana elimu ya uraia na ni vyombo vinavyoendeshwa kwa oder za wakubwa. Ni muhimu sana kwa chama mbadala kama Chadema Tanzania kuwa na watu kila idara kwa idadi kubwa katika vyombo vya usalama maana hivyo vyombo ndivyo vinavyotumika kulinda maslahi ya siasa za nchi.
#Mytake Tunahitaji Siasa Huru kutoka kwa wanasiasa Huru kwenda kwa Wananchi Huru wanaoweza kufanya maamuzi Huru katika nchi Huru ndio maana tunahitaji kutengeneza vyama Huru.
Asanteni sana