Wanasema kazi ya kulea mtoto ni kazi ya kijiji. Binafsi sina huwakika na maana halisi ya msemo huo. Sababu ya kusema hivyo ni kwamba, waliotunga hawa kufafanunua mwisho wa mipaka ya malezi hayo ambayo kijiji kinapaswa kumpa mtoto, haswa ukiwa hauna huusiano wowote na mtoto huyo.
Kwa mfano, ni vizuri kusaidiana, lakini sidhani kama kuna mzazi atakubali kuona mtoto wake anapewa zawadi kila kukicha na watu tofauti tofauti kisa “mtoto analelewa na kijiji.” Tafakari kidogo, unajua kiundani wewe unaweza kuhisi kuwa mnyonge (it will lower your self-esteem) kwani huwezi kutimiza mahitaji ya mwanao. Pili every human being needs to be a part of something (sense of belonging). Hivyo mazowea ya kuacha mtoto kupewa zawadi na kila mtu mtoto anaweza jenga tabia ya kuamini kuwa yeye ni mali ya kijiji, hivyo akashindwa kujidhamini.
Mfano wa pili ni pale kunapo kuja swala la kumkanya mtoto pale anapo kosea. Je wewe kama mzazi utakubali mtoto wako sio tu kugombezwa, bali kuchapwa na mtu baki? Saa nyingine wewe ni mmoja wa wazazi ambao hawaamini katika uchapaji wa watoto, halafu ukute jirani yako (ambaye ana amini kwenye dhana ya kuchapa watoto) kamchapa mtoto wako, utajisikiaje? Mtoto ni kweli amekosea na alihitaji kumkanywa lakini yeye akashika fimbo na kumchapa, kwasababu yeye ndivyo aleavyo. Hapo hapo kwenye swala la kukanya na kuadhibu watoto. Je wewe utakubali ndugu, au jirani yako ambaye hana mtoto amuadhibu mwanao?
Sasa wapendwa, ni nini haswa maana ya msemo huu “mtoto ulelewa na kijiji?” Na jinsi dunia ilivyo badilika utaki mtoto wako kuamini kila mtu. Angalau zamani ilikuwa rahisi kumwambia mtoto amini kila mtu, lakini siku hizi kitu cha kwanza unataka kumfundisha mtoto ni kuto amini kila mtu. Hata wale ambao wanaonekana well educated na public figure, kwasababu statistic za case za ubakaji na kulawiti watoto inaonyesha kuna wachungaji, mashehe, CEOs, wafanya biashara, majirani, wafanyakazi wako wa ndani, hata watu mashuhuri kwenye jamii. Watoto wengi ubakwa na kulawitiwa na watu ambao wana wafahamu na kuwaamini sana.
Msemo ulikuwa mzuri tu kwa zamani hizo ambazo wanajamii waliishi kama ndugu wa damu ila kwa sasa dunia imebadilika hasa na huu utandawazi, mathalan kwa zamani hizi imani inapotea siyo kwa wanakijiji tu ila hata kwa ndugu wa damu au jamii Moja!!!! Mungu atukuzie watoto wetu
Amen!